Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa meno(meno kuuma)chanzo,dalili na tiba



 UGONJWA WA MENO(MENO KUUMA)CHANZO,DALILI NA TIBA

Zipo sababu mbali mbali zinazochangia meno kuuma au mtu kuwa na matatizo mbali mbali ya meno,japo kwa asilimia kubwa ya watu hupata shida ya meno kwa sababu ya mashambulizi ya vimelea vya magonjwa kama vile bacteria n.k

MATATIZO MBALI MBALI YANAYOWEZA KUSUMBUA MENO YAKO NI PAMOJA NA;

1. Shida ya meno kubadilika rangi mfano meno kuwa na rangi ya njano, utando mweusi n.k soma zaidi hapa kuhusu meno kuwa na shida ya utando mweusi

2. Shida ya meno kufa ganzi,hii hutokea kwa watu wengi hasa kwenye mazingira ya joto sana au baridi kali sana,au kwa watu wanaopenda kula vyakula vyenye sukari nyingi,vichachu sana n.k

3. Shida ya meno kuoza yaani teeth decay,ambapo huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile fizi kulegea sana,fizi kutoa damu,usaha n.k

4. Shida ya meno kwenye fizi,kama vile fizi kutoa damu zenyewe,fizi kuwa na vidonda,fizi kutoa usaha n.k

5. Shida ya meno kusagika yenyewe,shida hii hutokea kidogo kidogo siku hadi siku,ambapo meno husagika kidogo kidogo wakati mtu akiwa amelala,akiwa na hisia kali,hasira kali ambayo huhusisha meno kugusana na kusagana n.k

6. Shida ya meno kutoboka yenyewe au kutengeneza vishimo, shida Hii huweza kuambatana na maumivu makali ya jino, na kwa asilimia kubwa meno kutoboka husababishwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile bacteria n.k

7. Shida ya meno kuchomoka yenyewe,meno huweza kutoka yenyewe au kutoka na kuacha vipande vilivyobaki kwenye fizi,hii pia ni shida ambayo huweza kuwapata baadhi ya watu,

CHANZO CHA MAGONJWA MBALI MBALI YA MENO NI PAMOJA NA;

- Mashambulizi ya vimelea mbali mbali ya magonjwa kama vile Bacteria n.k

- Mtu kutokusafisha meno pamoja na mdomo vizuri kila siku (poor hygiene)

- Ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi pamoja na mafuta mengi kila siku

- Mgonjwa wa sukari kushindwa kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu

- Swala la uvutaji wa sigara,tumbaku(tobacco),ugoro n.k

- Matumizi ya pombe kupita kiasi hasa pombe za kienyeji

- Magonjwa mbali mbali yanayohusu upungufu wa kinga mwilini kama vile UKIMWI,n.k

- Matumizi ya baadhi ya dawa zenye kemikali kali mdomoni n.k

DALILI ZA MATATIZO MBALI MBALI YA MENO NI PAMOJA NA;

• Mtu kupata maumivu makali ya jino au meno

• Mtu kupata shida ya meno kufa ganzi

• Mtu kupata shida ya fizi kutoa damu,kulegea,kuwa na vidonda,kutoa usaha n.k

• Mtu kupata shida ya meno kulegea,kuachana,kutoka yenyewe

• Mtu kuanza kutoa harufu mbaya mdomoni,puani n.k

• Mtu kupata shida ya meno kubadilika rangi n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments