UGONJWA WA MYCETOMA (MGUU WA MADURA),CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE
Mycetoma ni ugonjwa ambao husababishwa na bacteria pamoja na Fangasi ambao huingia mwilini kupitia kwenye ngozi iliyo na upenyo maeneo ya miguuni.
Bacteria wanaosababisha ugonjwa wa Mycetoma hujulikana kama ACTINOMYCETOMA na Fangasi wanaosababisha Ugonjwa wa Mycetoma hujulikana kama EUMYCETOMA.
Mara nyingi ugonjwa huu hushambulia ngozi na tishu laini maeneo ya miguuni, hasa mguu mmoja peke yake,Ugonjwa huu hushambulia mtu wa umri wowote ila kwa asilimia kubwa wanaume huonekana kushambuliwa zaidi ya wanawake, Pia miongoni mwa watu ambao huathirika zaidi na ugonjwa huu ni pamoja na Wakulima na Wafugaji.
Hakuna takwimu za moja kwa moja kwamba ugonjwa wa mycetoma umeathiri watu wangapi Duniani mpaka sasa,ila Kuna wastani wa Cases 17,607 ambazo ziliripotiwa mwaka 2017 katika "Review of Scientific articles ya mwaka 1950 na 2017"
VISABABISHI VYA UGONJWA WA MYCETOMA(MGUU WA MADURA)
Kama nilivyokwisha kuelezea hapo juu,Ugonjwa wa Mycetoma husababishwa na Bacteria ambao hujulikana kama ACTINOMYCETOMA pamoja na Fangasi wanaojulikana kama EUMYCETOMA.
Kwa ujumla miongoni mwa vimelea vinavyosababisha ugonjwa huo ni pamoja na; Madurella mycetomatis, Nigrograna mackinnonii, Trematosphaeria grisea (formerly Madurella grisea), Falciformispora senegalensis, Medicopsis romeroi, Pseudoallescheria boydii/Scedosporium apiospermum), Acremonium falciforme na Fusarium solani. Vimelea hawa huishi au hupatikana katika udongo na humuingia mtu kupitia mipasuko midogo midogo kwenye mguu ambao mtu anaweza kupata endapo akichomwa na miiba,vifuu,au kitu chochote katika eneo la kazi.
DALILI ZA UGONJWA WA MYCETOMA(MGUU WA MADURA) NI PAMOJA NA;
- Mgonjwa kuwa na vijinundu nundu (subcutaneous nodules) katika ngozi ambavyo mwanzoni haviumi lakini vinaongezeka ukubwa kadiri siku zinavyokwenda
- Baada ya muda, vijinundu hivo huanza kuungana na kutengeneza uvimbe mkubwa (tumors) katika eneo husika
- Uvimbe huu unaweza kutengeneza usaha kwa maana ya kua jipu (necrotic abscesses) na baadae kuanza kutokea vijinjia vidogo vidogo (draining sinus tracts) ambavyo vinakua vinatoa maji maji au usaha kutoka ndani ya uvimbe uliopo kwenye mguu husika.
- Kama hali hii isipotibiwa ugonjwa huzidi kua mkubwa,uvimbe huzidi kuongezeka na hatimae mguu unaweza kuharibika kabisa (uharibifu wa kudumu). Wakati mwingine hali hii inaweza kuingia ndani kabisa na kuhusisha nyama za ndani,mishipa ya damu na limfu na mifupa.
- Baada ya vijinundu kuwa vikubwa zaidi huweza kugeuka na kuwa vidonda yaani Oozing Sores
- Na pia kama mgonjwa hakupata tiba,ugonjwa huu wa mycetoma huweza kusambaa kutoka mguuni kwenda maeneo mbali mbali ya mwili wake
NAMNA UGONJWA WA MYCETOMA(MGUU WA MADURA) HUGUNDULIKA
Ugonjwa Huu wa mycetoma huweza kugundulika kupitia;
• Kuchukua historia yake kutoka kwa mgonjwa
• Kuangalia kwa macho eneo lililoathirika na ugonjwa huu
• Kuchukua vipimo vya maabara kama vile Biopsy,Damu n.k
• Kufanyiwa kipimo cha X-ray, Ultrasound au vipimo vya mionzi ili kuweza kuona kiundani maneo ya ndani kama kwenye viungo, mifupa n.k.
MATIBABU YA UGONJWA WA MYCETOMA(MGUU WA MADURA)
Mgonjwa huweza kupata tiba mbali mbali kulingana na chanzo cha ugonjwa pamoja na hali yake kwa wakati huo,na endapo mgonjwa ataanza tiba mapema hupona vizuri kabsa kwa haraka zaidi,
Matibabu ya ugonjwa huu wa mycetoma ni pamoja na kutumia dawa jamii ya Antibiotics kama umesababishwa na Bacteria(Actinomycetoma) pamoja na matumizi ya dawa jamii ya antifungal kama chanzo chake ni fangasi(Eumycetoma).
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!