magonjwa ya watoto
Ugonjwa wa Kupooza,Ugonjwa Wa Polio-Poliomyelitis(KUPOOZA MIGUU)
Ugonjwa wa Polio,chanzo,dalili na Tiba yake
Ugonjwa wa Polio (Poliomyelitis) au Ugonjwa wa Kupooza ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vinavyoitwa poliovirus. Ugonjwa huu huathiri zaidi watoto walio chini ya miaka mitano, ingawa mtu yeyote ambaye hajapata chanjo anaweza kuambukizwa. Virusi hushambulia mfumo wa neva na vinaweza kusababisha kupooza kwa kudumu, ulemavu au hata kifo katika baadhi ya wagonjwa.
POLIO ni ugonjwa wa kupooza ambao upo kwenye kundi la High Infectious Viral Disease, Ugonjwa huu huwapata sana Watoto wenye umri wa chini ya MIAKA MITANO(5),
Jinsi Polio Huenea
Polio huenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine hasa kupitia njia ya kinyesi kwenda mdomoni (faecal-oral route). Maambukizi yanaweza pia kutokea kwa kula chakula au kunywa maji yaliychafuliwa na virusi. Usafi duni wa mazingira na kutonawa mikono huongeza hatari ya maambukizi.
Virusi wa Polio huweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa Mwingine kwa njia ya Faecal-Oral pamoja na njia nyingine kama vile Contaminated water or Food.
Baada ya virusi hawa huingia kwa njia ya mdomoni moja kwa moja na kuanza kuzaliana sana kwenye Utumbo, na hapo ndipo huanza kusambaa maeneo mengine kama vile kwenye mfumo wa fahamu(Nervous system) na kusababisha tatizo la Kupooza(Paralysis) n.k.
Dalili za Polio
Watu wengi walioambukizwa wanaweza wasionyeshe dalili yoyote. Wengine hupata:
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass,Kama unachangamoto yoyote ya kiafya;Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatSapp,Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp Hapa- Homa
- Uchovu
- Maumivu ya kichwa
- Kutapika
- Kukakamaa kwa shingo
- Maumivu ya mikono na miguu
Katika visa vichache, virusi hushambulia mfumo wa neva na kusababisha kupooza, mara nyingi kwenye miguu. Kupooza huku kunaweza kuwa kwa kudumu.
DALILI ZA UGONJWA WA POLIO NI PAMOJA NA;
– Joto la mwili kuwa juu sana au kuwa na homa
– Uchovu wa mwili kupita kiasi
– Maumivu makali ya kichwa mara kwa mara
– Kupata shida ya kichefuchefu pamoja na Kutapika
– Kupatwa na shida ya Sore throat
– Shingo kukakamaa(neck stiffness)
– Maumivu ya Miguu
– Misuli ya mwili kuwa dhaifu sana
– Tatizo la kupooza kabsa hasa miguuni, kisha kumsababishia mtu ulemavu wa kudumu.(Ulemavu wa maisha).
MATIBABU YA UGONJWA WA POLIO
Mpaka sasa hakuna tiba yoyote ya kutibu kabsa ugonjwa huu wa Polio, Ila kuna CHANJO ya kuzuia ili mtu asipatwe na ugonjwa huu mbaya wa Polio.
Ndyo maana Wataalam wa afya tunasisitiza kwa nguvu zote watoto wote chini ya miaka 5 Wawe wameshapata chanjo hii.
Kinga na Tiba
Hakuna tiba inayoweza kuponya polio. Njia bora ya kujikinga ni kupata chanjo ya polio kwa dozi zote zinazopendekezwa. Wagonjwa hupatiwa huduma za kupunguza dalili, mazoezi ya viungo (physiotherapy), na huduma za urekebishaji ili kuboresha uwezo wa kutembea na kufanya shughuli za kila siku.
Facts Check:
Polio ni ugonjwa hatari lakini unaozuilika kwa chanjo. Kuimarisha chanjo kwa watoto, kudumisha usafi wa mazingira na kunawa mikono mara kwa mara ni hatua muhimu za kuzuia maambukizi. Ushirikiano wa jamii na huduma za afya una mchango mkubwa katika kutokomeza ugonjwa huu duniani.
References (Marejeo)
- World Health Organization (WHO). Poliomyelitis (Polio). https://www.who.int/health-topics/poliomyelitis
- World Health Organization (WHO). Poliomyelitis: Questions and Answers (2025).
- Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Learn About Polio Factsheet.
- World Health Organization Regional Office for Africa. Polio.
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa

