Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa Wa Saratani Ya Matezi(Lymphoma)



 UGONJWA WA SARATANI YA MATEZI(LYMPHOMA),CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

Saratani ya Matezi ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Lymphoma, Kuna aina kuu mbili za saratani hii ambazo hujulikana kama; (i) Hodgkin's Lymphoma (ii) Non-Hodgkin's Lymphoma.

Ripoti ya WHO(Shirika la Afya Duniani) mwaka 2020: Inasema kwamba,Kuna takribani watu milioni 10 ambao walipoteza maisha mwaka 2020 kutokana na aina hii ya Saratani ya Matezi.

CHANZO CHA SARATANI YA MATEZI

Hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea kwa ugonjwa huu,ila baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba, Kutokea kwa Kidonda kwenye DNA za aina ya Seli nyeupe ya Damu ambayo ni Lymphocyte,

Hapo ndipo lymphocyte hubadilika na kuwa seli hizi za Lymphoma(ambazo huungana na kuzalisha seli nyingi zaidi zenye Viuvimbe)

DALILI ZA SARATANI HII YA MATEZI NI PAMOJA NA;

- Uvimbe wa tezi la limfu usiyo na maumivu yoyote,

tezi hili la limfu lipo maeneo mbali mbali ya mwili wako kama vile;

• Kwenye vidole vyako

• Sehemu za siri

• Maeneo ya kwapani

• Maeneo ya Shingoni

• Nyuma ya masikio

• Nyuma kichwa N.k

- Joto la mwili kuwa juu sana au Mgonjwa kuwa na homa

- Mgonjwa kutokwa na jasho sana wakati wa usiku

- Kupata uchovu sana wa mwili

- Mgonjwa kupatwa na hali ya kikohozi

- Mgonjwa kupatwa na shida ya kuwashwa mwilini

- Mgonjwa kupata shida ya kupumua au kukosa pumzi

- Mgonjwa kupungua uzito kwa kasi sana n.k

VIHATARISHI VYA KUPATWA NA SHIDA HII YA SARATANI YA MATEZI NI PAMOJA NA;

• UMRI; kuwa na umri wa kati ya miaka 20,40 au zaidi ya 60

• JINSIA; Wanaume wapo kwenye hatari zaidi kuliko wanawake

• KINGA YA MWILI; Watu wenye kinga ndogo ya mwili

• MAGONJWA MENGINE; Watu ambao wamepatwa na maambukizi ya magonjwa mengine kama vile; Epstein Barr Virus,maambukizi ya Helicobacter pylori n.k

VIPIMO:

- Dalili,historia ya ugonjwa pamoja na mgonjwa kuchunguzwa yaani physical examination

- Mgonjwa kuchukuliwa sample ya Lymph node kwa ajili ya uchunguzi zaidi

- Vipimo vya damu yaani Blood tests

- Mgonjwa kuchukuliwa sample ya Bone Marrow

- Vipimo vingine ni kama vile,CT Scan,MRI n.k

MATIBABU YA UGONJWA WA SARATANI YA MATEZI

✓ Matibabu ya Saratani hii hutegemea na hatua au stage ya ugonjwa, Na mtu hupata tiba nzuri na kupona haraka zaidi kama saratani hii imegunduliwa mapema zaidi au kwenye hatua za mwanzoni,

Baadhi ya matibabu ni pamoja na;

1. Huduma ya chemotherapy

2. Huduma ya mionzi au Radiotherapy

3. Huduma ya Bone marrow transplant n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments