Uhusiano wa Usugu wa dawa na magonjwa ya figo,Prof. Jeremiah aeleza
Uhusiano wa Usugu wa dawa na magonjwa ya figo,Prof. Jeremiah aeleza
#Picha:Prof. Jeremiah Seni, Profesa Mshiriki wa Vimelea vya Magonjwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya Bugando, Mwanza Tanzania.
Viongozi wa Umoja wa Mataifa wakutana jijini New York, Marekani kujadili hatua za kudhibiti hatari itokanayo na usugu wa vimelea dhidi ya dawa, UVIDA au kwa kiingereza AMR, nchini Tanzania mtaalamu wa suala hilo amedadavua uhusiano kati ya usugu wa dawa na magonjwa kama vile figo na maambukizi katika njia ya mkojo, UTI.
Katika mahojiano na Jeremiah Seni, Profesa Mshiriki wa Vimelea vya Magonjwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya Bugando, Bosco Cosmas wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa alimuuliza hasa chanzo na madhara ya usugu wa dawa hizo.
Usugu dhidi ya vimelea vya magonjwa ni hali ambayo vimelea wanaosababisha magonjwa mbalimbali, wanafanya mabadiliko na hivyo kukinzana na dawa ambazo awali zilikuwa zinatumika kuwatibu, na vimelea hawa tunawagawa katika makundi Matano ambayo tuna bakteria, virusi, fangasi, minyoo na jamii zingine za parasaiti kama wale wanaosababisha malaria.
UTI isipotibika inaposababisha magonjwa ya figo
Ingawa watu wengi wameishi na tatizo hili la usugu bila kufahamu, lakini athari zake ziko wazi kwa afya ya umma, nikamuuliza Prof. Seni kuwa usugu unawezaje kuathiri afya ya umma? Profesa Seni akachambua zaidi akisema, “tukiachana na haya magonjwa ambayo serikali yamejiwekea mpango mkakati wa kupambana nayo kama UKIMWI, kifua kikuu na malaria mgonjwa anapopata maambukizi maana yake ule ugonjwa utakaa muda mrefu zaidi kwa hiyo inawezekana mtu alikuja na maambukizi tu kwenye njia ya mkojo (UTI) ni kawaida lakini kama ana usugu maana yake anaweza akachelewa kupona na pia kusababisha mgonjwa kupoteza maisha na kuongezeka kwa gharama za matibabu.”
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, UVIDA husababisha vifo vya watu 700,000 kwa mwaka, lakini wanatabiri kuwa hadi ifikapo mwaka 2030, linaweza kusababisha vifo vya takribani watu milioni 10. Nikamuuliza nini kifanyike tatizo hili lisiwe na madhara zaidi kwa watu ulimwenguni?
Ukiangalia takwimu ni kweli kabisa mwaka 2014 utafiti mkubwa kabisa uliosimamiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni ambao uliangalia zaidi vifo vinavyotokana na UVIDA na walifanya makisio ya wale watu takribani 700,000 wamepoteza maisha kutokana na UVIDA na mbaya zaidi robo tatu ya vifo hivyo ni kutoka bara la Afrika na Kusini mashariki mwa bara la Asia kwahia vifo hivyo ni kutoka bara la Afrika na Kusini mashariki mwa bara la Asia kwahiyo ni vyema kwa serikali kuona ukubwa wa tatizo hili na kuwekea mkazo katika mapambano kama walivyoweka kwa magonjwa mengine makubwa.”
Wafamasia wanachukua hatua gani kudhibiti UVIDA?
Moja kati ya sehemu muhimu ambayo inaweza kusaidia kupunguza ama kumaliza tatizo hili ni katika maduka ya dawa ambapo mara nyingi wagonjwa huwa wanaenda kununua dawa bila kufuata taratibu za vipimo. Clinius Amani Caroly, Mteknolojia dawa katika hospitali ya Mwananchi iliyopo mkoani Mwanza, anaeleza hatua wanazochukua katika utoaji wad awa kwa mgonjwa.
Sasa kwa utoaji wa dawa kwa mgonjwa ambaye hana karatasi ya daktari, kuna makundi mawili, kwanza kwa kitaalamu kuna kitu kinaitwa over the counter medicine, ambazo ni dawa zinazoweza kutolewa kwa mgonjwa bila karatasi ya daktari lakini pia kuna prescription medicine ambazo mgonjwa akija bila karatasi ya daktari hatuwezi kumpatia. Mgonjwa anapokuja bila karatasi ya daktari kwanza tunajiridhisha kama kweli dawa anayotaka inaendana na ugonjwa wake na tunawapa ushauri wa Kwenda kumuone daktari.
Muathirika wa UVIDA na hatua alizochukua sasa
Je, wahanga wana uelewa kuhusu namna sahihi ya kukabiliana na usugu? Neema Gervas, muhanga wa tatizo hili anaeleza nini anafanya anapogundua amepata usugu.
“Kwa upande wangu suala la usugu wa dawa limenitesa kwa muda mrefu sana kwasababu hapo awali nilikuwa natumia hizi dawa za kutuliza maumivu hasa ninapohisi maumivu ya kichwa lakini kwa sasa nikitumia haisaidii kupata unafuu. Nilienda phamasi nikawaambia dawa ambazo huwa ninatumia hazinisaidii kwahiyo wananishauri kubadilisha daw ana nikawa napata nafuu.” Via;UN
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!