Umuhimu Wa Kwenda Hospital(Ukiumwa Wahi Hospital)

 UMUHIMU WA KWENDA HOSPITAL(ukiumwa wahi hospital)

Ni tabia ya watu wengi kutokukimbilia hospital pale wanapohisi kuumwa,na wengi wao hufika hosptal pale tatizo linapokuwa kubwa zaidi au wanapofikia hatua mbaya ya kushindwa kufanya kitu chochote.

UMUHIMU WA KWENDA HOSPITAL(ukiumwa wahi hospital)

- Kila ugonjwa hutibika haraka endapo umegundulika mapema,mfano; kansa au saratani,tatizo hili huweza kutibiwa kabsa na mtu kurudi katika hali yake ya kawaida endapo limegundulika mapema,

- Kujua aina ya ugonjwa unaokusumbua,chanzo chake,dalili zake zote pamoja na kupata tiba ya tatizo lako

- Vipimo vya kila aina ya ugonjwa utavipata hosptalini,hivo nenda hospitalini kwa ajili ya kufanya full checkup

- Sio kila homa ni Malaria,hivo ukienda hospitalini utajua ni tatizo gani linakusumbua na kuepuka matumizi ya dawa hovio kwa kuhisi aina ya ugonjwa ambao unakusumbua

- Matumizi ya dawa bila ushauri kutoka kwa wataalam wa afya au bila kufanyiwa vipimo ni hatari kwa afya yako

BAADHI YA VIPIMO MUHIMU KWA WAGONJWA WAKIFIKA HOSPTAL NI PAMOJA NA:

• Kipimo cha Presha au shinikizo la damu

• Kipimo cha joto mwili

• Kipimo cha damu au Full blood picture(FBP)

• Kipimo cha oxygen yaani oxygen concentration

• Kipimo cha mapigo ya moyo

• Pamoja na vipimo mbali mbali kama Ultrasound,X-Ray, n.k kulingana na dalili za ugonjwa ulio nayo

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!