UTANDO MWEUSI KWENYE MENO
Meno hupata rangi yake ya asili kwa asilimia kubwa kutokana na uwepo wa Calcium, lakini kwa namna moja au nyingine rangi hii nyeupe asilia ya meno huweza kubadilika na kuwa nyeusi au kutengeneza dots nyeusi n.k kutokana na sababu mbali mbali,
Kuna baadhi ya watu wana hii shida ya kuwa na utando mweusi kwenye meno bila wao kujua chanzo ni nini? au wengine hata hawajui kwamba wana shida hii,
CHANZO CHA UTANDO MWEUSI KWENYE MENO NI PAMOJA NA;
- Usafi duni wa meno na kinywa kwa ujumla yaani poor hygiene
- Uvutaji wa sigara au matumizi ya tumbaku/tobacco huweza kufanya meno kuwa meusi pamoja na kufanya fizi za meno kuwarahisi kushambuliwa na magonjwa mbali mbali
- Matumizi ya vinywaji vyenye rangi nyeusi kwa asilimia kubwa kama vile; chai ya rangi, kahawa,coca cola au Red wine huweza kuleta utando mweusi kwenye meno
- Tatizo la jino kuharibika au kuoza pamoja na fizi zake
- Tatizo la damu kutoka kwenye fizi, Damu kutoka kwenye fizi huweza kuingia kwenye meno na kusababisha kutengeneza utando kwenye meno
- Maambukizi ya magonjwa mbali mbali ya meno
- Uwepo wa vishimo kwenye meno kutokana na mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria,vishimo hivi huweza kutengeneza weusi kwenye meno yote yaliyoathiriwa
- Huduma ya kuziba meno(dental restoration) yenye shida kwa kutumia njia mbali mbali kama vile; zinazohusisha matumizi ya Silver Sulfide huweza kubadilisha rangi ya meno na kutengeneza utando mweusi
- Matumizi ya baaadhi ya dawa kama vile; dawa jamii ya Liquid Iron supplements huweza kusababisha utando mweusi kwenye meno
- Tatizo la Tartar(hard plaque deposits) ambapo huhusisha kitu kigumu kujijenga kwenye meno hasa chini ya fizi na kuwa cheusi, N.k
KUMBUKA; Shida hii ya meno kutengeneza utando mweusi huanza kidogo kidogo kama spots ambazo huonekana rangi ya kijivu au Brown na baadae kuwa rangi nyeusi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!