Uvimbe Kwenye Figo,chanzo,dalili,tiba

 UVIMBE KWENYE FIGO,CHANZO,DALILI,TIBA

Uvimbe kwenye figo(kidney mass or tumor), uvimbe huu ukiwa mkubwa zaidi huweza kuwa ni kiashiria mojawapo cha uwepo wa tatizo la kansa kwenye figo yaani kidney cancer,

Japo sio mara zote, leo katika makala hii tunachambua kuhusu chanzo,dalili na Tiba ya uvimbe kwenye Figo

CHANZO CHA UVIMBE KWENYE FIGO

- Hakuna sababu ya moja kwa moja inayohusishwa na tatizo hili,Japo zipo sababu ambazo zimeonekana kuongeza kwa kiasi kikubwa watu kupatwa na tatizo hili la uvimbe kwenye figo, Na sababu hizo ni kama vile;

1. Uvutaji wa sigara

2. Unywaji wa Pombe kupita kiasi

3. Shida ya uzito mkubwa kupita kiasi,unene au Obesity

4. Kutokula mlo kamili mara nyingi pamoja na kula vyakula vya mafuta zaidi

5. Mtu kuwa na shida ya Presha

6. Kuwepo kwenye huduma ya Kidney Dialysis kwa muda mrefu zaidi

7. Kufanya kazi kwenye mazingira yenye chemicals zenye Chlorine zaidi.

8. Kupata vinasaba vya shida hii kwenye familia, Inasemekana asilimia 4-6% ya shida hii huweza kuchangiwa na sababu hii ya kurithi vinasaba vya tatizo kutoka kwenye Familia yako N.k

DALILI ZA TATIZO LA UVIMBE KWENYE FIGO NI PAMOJA NA;

- Mtu kuanza kukojoa damu yaani kwa kitaalam hematuria

- Kupatwa na maumivu makali kati ya mbavu na Hips

- Kupatwa na maumivu makali chini ya mgongo upande mmoja,ambayo hayaishi

- Kukosa kabsa hamu ya kula chakula

- Kuonyesha dalili zote za kupungukiwa na damu au anemia,kama vile ngozi ya viganja vya mkono,machoni na kwenye lips za mdomo kuwa nyeupe zaidi kuliko kawaida

- Uzito wa mwili kupungua kwa kasi zaidi

- Kupatwa na homa au joto la mwili kuwa juu zaidi mara kwa mara N.k

VIPIMO AMBAVYO HUWEZA KUFANYIKA:

-Kuchukua historia ya ugonjwa pamoja na physical examination

- Kufanya Complete Blood Count(CBC)

- Urinalysis

- Serum Creatinine Levels checking

- CT scan, MRI

- Kidney Mass Biopsy N.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

• Zipo tiba mbali mbali kulingana na chanzo husika pamoja na ukubwa wa tatizo,ila kwa ujumla kuna matumizi ya dawa mbali mbali pamoja na Tiba ya Upasuaji.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!