Ticker

6/recent/ticker-posts

Vidole vya mikono kufa GANZI(Chanzo chake)



 VIDOLE VYA MIKONO KUFA GANZI(Chanzo chake)

Watu wengi hupatwa na tatizo hili la vidole vya mikono kufa ganzi, kwa kuliona hilo,leo nmekuletea baadhi ya sababu za tatizo hili, soma hapa;

1. Ugonjwa wa kisukari, hapa nazungumzia Diabetes neuropathy, ambapo baada ya ugonjwa wa kisukari kutokea huharibu nerves hasa kwenye maeneo ya miguuni na mikononi,

ndyo maana wagonjwa wengi wa kisukari hupatwa na tatizo hili la vidole vya mikono pamoja na miguu kufa ganzi.

2. Matatizo yote ambayo yanahusu kuharibiwa kwa nerves kwenye maeneo ya shingoni, mikono na miguuni kama vile; Carpal tunnel,Cervical radiculopathy,Ulnar nerve entrapment n.k

3. Tatizo la Raynaud's Disease, Huu ni ugonjwa ambao husababisha mishipa ya ARTERIES Kwenye mikono kuwa mwembamba zaidi,hali ambayo hupunguza flow ya damu kwenye nerves zilipo kwenye mikono ikiwemo na vidole,

Hii husababisha upungufu wa damu kwenye nerves kisha kupelekea vidole pamoja na mikono kuanza kupata tatizo la ganzi.

4. Hali ya baridi sana, hali hii ya baridi sana huweza kusababisha mpaka vidole vya mikono kufa ganzi, japo haidumu kwa muda mrefu sana tatizo hili huondoka lenyewe

5. Shida ya Emotional Distress, kuna baadhi ya watu wakiwa kwenye hali isiyo na utulivu kihisia huweza kupata pia shida ya vidole kufa ganzi.

6. Vidole vya mikono kubanwa sehemu kwa namna yoyote ile kama kukaliwa, n.k

7. Tatizo la Rheumatoid arthritis(RA), hii ni autoimmune disordrer ambayo huweza kuleta uvimbe,maumivu kwenye joints, ganzi kwenye vidole vya mikono, hali ya kuungua kwenye mikono n.k

8. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali(INFECTIONS) huchangia japo kwa kiwango kidogo, maambukizi hayo ni kama vile;

- Lyme disease: ugonjwa unaosababishwa na Bacteria kisha kusambazwa na TICKS

- Kaswende(syphilis): ugonjwa wa zinaa ambao huweza kuathiri mfumo wa fahamu

- Ukimwi(HIV/AIDS): maambukizi ya ukimwi pia huweza kuharibu nerves kisha kuchangia tatizo hili.

- Ukoma(Hansen's disease or Leprosy):Maambukizi ya bacteria kwenye ngozi,nerves pamoja na misuli

9. Vitu vyote ambavyo huweza kuathiri mishipa ya damu pamoja na Nerves kama vile; Myloidosis,Guillain-Barre's syndrome,Multiple sclerosis,Vasculitis,Fibromyalgia,Stroke,Thoracic outlet syndrome n.k

10. Sababu zingine ni kama vile;

- Madhara ya dawa mbali mbali kama vile chemotherapy drugs n.k

- Shida ya ganglion cyst

- Upungufu mkubwa wa Vitamin B12 n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments