Vijana wanaoishi na VVU wapaza Sauti Zao Duniani ili kutokomeza UKIMWI

Vijana wanaoishi na VVU wapaza Sauti Zao Duniani ili kutokomeza UKIMWI

Vijana wawili wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii na pia wanaishi na Virusi Vya Ukimwi, VVU wanakwenda New York, Marekani kushiriki vikao vya ngazi ya juu vya Umoja huo ukiwemo Mkutano wa Zama Zijazo, SOTF na Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu, UNGA79.

Vijana hao si wengine bali ni Ibanomonde Ngema kutoka Afrika Kusini na Jerop Limo kutoka nchini Kenya ambao kwa pamoja watawaeleza viongozi wa dunia umuhimu wa kushirikiana na vijana katika kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

“Watatoa wito kwa viongozi kuwekeza kwenye mifumo rafiki ya afya kwa vijana, na kutoa huduma kamilifu kwa vijana wanaoishi na VVU, na vile vile kushirikiana na vijana na jamii ili kuwawezesha kuongoza hatua dhidi ya UKIMWI,” imesema taarifa ya UNAIDS iliyotolewa Geneva, Uswisi na New York, Marekani leo Alhamisi Septemba 19.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima amenukuliwa kwenye taarifa hiyo akisema uanaharakati wa vijana ulioajaa bashasha na nguvu umechochea maendeleo makubwa kwenye hatua dhidi ya UKIMWI.

“Wanafahamu ni jambo gani linawafaa. Ni muhimu sana kwa viongozi kuwasikiliza na kuelewa changamoto mahsusi ambazo vijana wanakabiliana nazo na ni kwa namna gani kuzikabili. Viongozi wanaweza kupanga vema jinsi ya kutokomeza UKIMWi na kusongesha maendeleo yaliyopatikana kwa kushirikiana na vijana wanaoishi na VVU,” amesema Bi. Byanyima.

Sauti zetu zijumuishwe kuanzia utungaji hadi utekelezaji wa sera - Jerop

Jerop akinulikuwa kwenye taarifa hiyo amesema “ninawakilisha sio tu sauti za wakenya milioni 1.5 wanaoishi na VVU bali watu wote wanaoishi na VVU. Ninataka viongozi waondoke New York wakitambua kuwa sisi sio wanufaika, bali ni watu wenye haki sawa. Tuna sauti, tuna stadi na utaalamu na tunahitaji jukwaa sawa ambako takwimu zetu zinaheshimika, ambako michango yetu inaheshimika na ambako sauti zetu zinasikika. Tunataka katika fursa zote za hatua dhidi ya UKIMWI kuweko na ushiriki wa vijana barubaru wenye maana na jumuishi kimaadili.”

Vijana, hasa barubaru wa kike na vijana wa kike wameathiriwa kwa kiasi kikubwa na VVU. Duniani kote mwaka 2023, asilimia 44 ya maambukizi mapya ya VVU ni miongoni mwa wanawake na wasichana na kila wiki wanawake vijana na wasichana 4000 duniani kote wanaambukizwa VVU, kati yao hao, 3100 wako nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara.

Tunajua jinsi ya kuishi kila siku na VVU - Ibanomonde

Ibanomonde Ngema, yeye anasema serikali zikikutana New York haziwezi kutokomeza UKIMWI peke yao. Zinapaswa kutushirikisha ili kusaka majawabu. Tumeishi na na VVU na tuna uzoefu wa kuishi na ugonjwa huo, kuanzia matibabu hadi afya ya akili, kwa sababu tunalazimika kusaka mbinu za kuishi na VVU kila siku.

Tunataka kujumuishwa kwenye utungaji wa sera ili tuweze kumiliki harakati za utokomezaji wa UKIWMI kama tishio la afya ya umma. Dunia inaweza kunufaika pindi vijana watakapojumuishwa kwenye hatua dhidi ya VVU. Hakuna mashauriano kuhusu VVU yanapaswa kufanyika bila kutujumuisha, kuanzia sera hadi utendaji mashinani.”

Limo ametamatisha akisema kutoa matibabu pekee haitoshi, vijana wanaoishi na VVU wanahitaji elimu na wanahitaji ajira ili waweze kuishi.

Via UN:

SOMA ZAIDI Hapa Kuhusu Ukimwi;....

kujikinga na ugonjwa hatari wa ukimwi. Hapa chini ni baadhi ya hatua za kuzuia maambukizi:

  • Kutumia Kondomu,Kutumia kondomu wakati wa kufanya ngono ni njia bora ya kuzuia maambukizi ya VVU. Kondomu huzuia muingiliano kati ya majimaji yanayoweza kuwa na VVU kutoka kwa mwenzi mmoja hadi mwingine.
  • Kuepuka Ngono Zisizo Salama,Ngono zisizo salama ni hatari kubwa kwako kupata VVU. Kuepuka ngono zisizo salama ni njia bora ya kuzuia maambukizi.
  • Kutumia vifaa vya ncha kali kama Sindano,nyembe n.k vikiwa Safi na pasipo kushirikiana na mtu mwingine
  • Kupata Vipimo vya VVU,Kupata vipimo vya VVU ni muhimu kwa kujua hali yako ya afya. Kwa kupata vipimo, unaweza kugundua mapema ikiwa una VVU na kupata matibabu haraka ikiwa inahitajika.
  • Kupata Matibabu ya VVU,Kupata matibabu ya VVU ikiwa ni pamoja na kutumia dawa za kurefusha maisha maarufu kama ARVs ni muhimu kwa kuzuia maambukizi zaidi ya ukimwi. Matibabu ya VVU husaidia kupunguza kiwango cha virusi katika mwili na kuongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.

Dalili za Ukimwi

Kwa asilimia kubwa baada ya maambukizi ya virusi vya ukimwi au HIV/AIDS,

Huchukua muda wa wiki 2 mpaka 4 kwa dalili kuanza kuonekana kwa mtu.

KUMBUKA: Vitu Hivi viwili, Kuna Window period pamoja na Incubation Period,

(i) Incubation Period-Tunazungumzia kipindi toka unapata maambukizi mpaka Dalili zinavyoanza Kuonekana,

ambapo huweza kuchukua muda wa wiki 2 mpaka 4 kwa dalili kuanza kuonekana kwa mtu.

(ii) window period- Ni Kipindi toka unapata maambukizi mpaka Muda ambao kipimo kinaweza kugundua/detect Virusi vya ukimwi-VVU ndani ya mwili wako.

Ambapo;

  • Antibody tests kwa kawaida vinaweza kutambua VVU siku 23 hadi 90 baada ya kuambukizwa. Vipimo vingi vya Rapid tests ni vipimo vya kutumia kingamwili.
  • Kipimo cha rapid antigen/antibody test kilichofanywa kwa kutoa damu kidoleni kwa kawaida kinaweza kutambua VVU kati ya siku 18 hadi 90 baada ya kuambukizwa.
  •  Kipimo cha maabara cha antigen/antibody lab test kwa kutumia damu kutoka kwenye mshipa wa VEIN kwa kawaida kinaweza kutambua VVU kati ya siku 18 hadi 45 baada ya kuambukizwa.
  • Na Kipimo cha nucleic acid (NAT) kwa kawaida kinaweza kutambua VVU siku 10 hadi 33 baada ya kuambukizwa.

DALILI HIZO ZA UKIMWI(HIV/AIDS)  NI PAMOJA NA;

1. Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na homa za mara kwa mara

2. Kupatwa na shida ya mafua ambayo hayaishi

3. Kupatwa na shida ya maumivu makali ya kichwa mara kwa mara

4. Kupatwa na maumivu ya misuli pamoja na joints

5. Mwili kuchoka sana kuliko kawaida

6. Mwili kuanza kuwa na rashes au Upele kwenye ngozi

7. Kutokewa na vidonda mdomoni,kooni,kupata maumivu wakati wa kumeza kitu,

8.Tezi za Lymph au lymph node kuanza kuvimba hasa eneo la shingoni n.k

9. Mtu kupatwa na tatizo la kuharisha

10. Mtu kutoa sana jasho kuliko kawaida

11. Uzito wa mwili kupungua kwa kasi zaidi(body weight loss)

12. Mtu kuanza kupatwa na kikohozi cha mara kwa mara n.k

NB: Kama unapata dalili kama hizi nenda hospital kufanya vipimo zaidi.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!