Vipimo Vya Ukimwi Vinaonyesha Negative Lakini Mtu Anaonyesha Dalili Zote Za HIV

 VIPIMO VYA UKIMWI VINAONYESHA NEGATIVE LAKINI MTU ANAONYESHA DALILI ZOTE ZA HIV

Kuna baadhi ya watu hukutana na changamoto hii,wamepima vipimo vya ukimwi,wamerudia baada ya miezi 3 mpaka 6,lakini majibu bado ni NEGATIVE na wana dalili zote au viashiria vyote vya maambukizi ya ukimwi,je hii ipoje?

SOMA HAPA KUJUA ZAIDI;

Baada ya mtu kupata maambukizi ya ukimwi mfumo wa kinga ya mwili huanza kutengeneza antibodies ambazo hujulikana kama HIV-antibodies,

Sasa kipindi cha kuanzia maambukizi ya virusi vya ukimwi mpaka mwili kutengeneza HIV-antibodies hujulikana kama SEROCONVERSION,ambapo hapa ndyo HIV-Antibodies huweza kugundulika kwenye mwili wako,

KATIKA KIPINDI HIKI CHA MAAMBUKIZI YA UKIMWI MTU HUWEZA KUANZA KUPATA DALILI MBALI MBALI KAMA VILE;

- Mtu kupata shida ya uchovu au Mwili kuchoka kupita kawaida

- Joto la mwili kuwa juu au Kupata homa za mara kwa mara

- Mtu Kupata madonda ndani ya koo au mdomoni kwa ndani

- Mtu kupata maumivu makali ya kichwa cha mara kwa mara

- Wengine kuanza kupata shida ya mafua ya mara kwa mara

- Kuvimba kwa lymph nodes au tonsils maeneo ya shingoni na kooni

- Ngozi ya Mwili kuanza kuwa na rashes n.k

(SEROCONVERSION) kipindi toka maambukizi ya virusi vya ukimwi mpaka mwili kutengeneza HIV-antibodies hutofautiana kati ya mtu na mtu kulingana na Uimara wa kinga yake ya Mwili pamoja na Aina ya vipimo vya ukimwi vilivyotumika kupima (HIV TESTS).

HIZI HAPA CHINI NI AINA ZA VIPIMO MBALI MBALI VYA UKIMWI

1. Nucleic acid tests(NATs)

Hapa kipimo hiki hupima na kugundua uwepo wa RNA Za Kirusi chenyewe cha ukimwi,

Kipimo hiki huweza kutoa majibu juu ya kiwango cha uwepo wa virusi vya ukimwi kwenye mwili wako yaani Viral load,

kipimo hiki ni cha garama sana kutumika

2. Antibody and antigen tests

Hiki ni kipimo cha Ukimwi au HIV ambacho hupima uwepo wa vitu viwili kwa pamoja yaani Hiv antigen maarufu kama P24 pamoja na uwepo wa HIV-antibodies kwenye mwili wako,

Hivo antigen za kirusi huweza kugundulika lakini pia mwili wako ukizalisha Antibodies yaani HIV- antibodies huweza kugundulika pia,
Kipimo hiki hutumika sana kwenye nchi zilizoendelea kama vile Marekani(USA) n.k

3. Antibody tests

Hiki ni kipimo cha ukimwi ambacho hupima tu uwepo wa HIV-antibodies kwenye mwili wako basi, tofauti na kipimo hicho cha juu ambacho hugundua antigen pamoja na antibodies,

Hapa ndyo mtu huweza kupimwa kwa kuchukuliwa sample ya Damu au mate mdomoni yaani oral fluid sample, japo damu hutumika zaidi kwani hutoa majibu kwa haraka zaidi kuliko kupima Maambukizi ya ukimwi kwa kutumia Oral fluid sample

VIPIMO VYA UKIMWI VINAONYESHA NEGATIVE LAKINI MTU ANAONYESHA DALILI ZOTE ZA HIV HII IPOJE?

Kama nilivyokwisha kusema hapo juu,(SEROCONVERSION) ni kipindi toka maambukizi ya virusi vya ukimwi mpaka mwili kutengeneza HIV-antibodies ambapo hutofautiana kati ya mtu na mtu kulingana na Uimara wa kinga yake ya Mwili pamoja na Aina ya vipimo vya ukimwi vilivyotumika kupima(HIV TESTS),

Hivo basi, dalili zote za ukimwi huweza kuonekana kwa mtu ila bado akipimwa huonekana hana maambukizi yoyote ya ukimwi yaani NEGATIVE kwani, ili kipimo kitoe majibu hutegemea na mfumo wa kinga yake ya mwili umetengeneza HIV-antibodies lini,

Hivo swala la dalili kuonekana huweza kuwahi zaidi,lakini uwepo wa HIV antibodies kwenye mwili wako ukachelewa zaidi,na kisha kupelekea hata majibu yako kuchelewa kupatikana,

KUMBUKA: Muda wa kawaida kwa mtu aliyepata maambukizi ya virusi vya ukimwi kuanza kuonyesha dalili kwenye mwili wake ni kuanzia wiki 2 mpaka 4,

Na muda wa kawaida kwa vipimo kuanza kuonyesha majibu yako ya maambukizi ya virusi vya ukimwi ni baada ya Miezi 3 toka siku ya maambukizi,ambapo hii ni kwa asilimia 98% ya Wagonjwa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE,TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!