Vitu Vinavyo Haribu Figo,Soma hapa

 VITU VINAVYO HARIBU FIGO

Kabla ya kuanza na vitu vinavyoweza kuharibu figo, Je ni dalili zipi zitajitokeza kwa mtu mwenye matatizo ya Figo?

HIVI HAPA CHINI NI BAADHI YA DALILI KWA MTU MWENYE MATATIZO YA FIGO

- Kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika mara kwa mara

- Kukosa kabsa hamu ya kula kitu chochote

- Kupatwa na shida ya kukosa Usingizi

- Mwili kuchoka kupita kiasi na kuwa dhaifu sana

- Mgonjwa kukojoa kojoa mara kwa mara kuliko kawaida

- Mgonjwa kukosa mkojo kwa muda mrefu au kukojoa mkojo mdogo sana

- Mgonjwa kupatwa na shida ya kukakamaa misuli ya mwili

- Mgonjwa kupatwa na tatizo la KUVIMBA MIGUU

- Ngozi ya mwili kukakamaa kuliko kawaida na wakati mwingine kupata miwasho

- Kupatwa na shida ya Presha kuwa juu mara kwa mara

- Kupatwa na shida ya kukosa pumzi,maumivu ya kifua n.k

VITU VINAVYO HARIBU FIGO NI PAMOJA NA

1. Mtu kuwa na ugonjwa wa Kisukari yaani Type 1 and 2 Diabetes

2. Mtu kuwa na shida ya Presha kuwa juu sana

3. Kuvimba kwa kichujio kwenye figo yaani Glomerulonephritis

4. Figo kushambuliwa na magonjwa mbali mbali kama vile Polycystic kidney disease n.k

5.Kupatwa na shida ya kuziba kwa njia ya mkojo kwa kipindi kirefu kutokana na,sababu mbali mbali kama vile kukuwa kwa tezi dume(enlarged prostate) n.k

6. Figo kushambuliwa na vimelea vya magonjwa ambavyo hujirudia mara kwa mara ndani ya muda mfupi

7. Kuwa na magonjwa mbali mbali ya moyo

8. Uvutaji wa Sigara

9. Unywaji wa Pombe kupita kiasi

10. Matumizi ya mara kwa mara ya baadhi ya dawa au matumizi ya dawa kwa dose kubwa kuliko kawaida

11. Tatizo la viribatumbo au kuwa na uzito mkubwa kuliko kawaida n.k

ZINGATIA MAMBO HAYA ILI KUJIKINGA NA MATATIZO MBALI MBALI YA FIGO

• Epuka kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha mafuta

• Hakikisha unapunguza uzito wako wa mwili

• Epuka matumizi ya Pombe kupita kiasi

• Epuka uvutaji wa Sigara

• Hakikisha unadhibiti kiwango cha sukari pamoja na Presha kwenye damu

• Hakikisha unafanya mazoezi ya mwili kila siku angalau kwa nusu saa(dakika 30)

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!