Vyakula 10 Bora kwa Mgonjwa wa Presha

Vyakula 10 Bora kwa Mgonjwa wa Presha

Kama wewe ni mgonjwa wa Presha, nikiwa na maana presha ya kupanda(High blood pressure),

Vyakula hivi hapa ni vizuri zaidi kwako;

1. Ndizi,

Ndizi ni chakula bora kwa ajili ya kushusha presha kwa mgonjwa wa presha,

Hii ni kwa Sababu ndizi zina Potassium, ambayo huweza kusaidia kushusha presha.

2. Kula matunda mbali mbali ikiwemo,

matunda jamii ya Citrus fruits,

  • Machungwa,
  • au tumia Strawberries n.k

3. Pendelea kula Tikiti maji, Tikiti maji lina Amino acid inayojulikana kama Citrulline,

Mwili hubadilisha Citrulline kuwa arginine ambapo matokeo yake hutengeneza nitric oxide, gesi ambayo husaidia kutanua mishipa ya damu, na hivo kusaidia kwa mtu mwenye shinikizo la juu la damu.

4. Matumizi ya Dark chocolate, Hii inaweza kuwa sio kitu kigeni kwako,

Kusikia kuhusu faida za chocolate ambayo ni dark chocolate,

Dark chocolate huweza kusaidia pia kwa mtu mwenye presha ya kupanda,

Kwani ina Flavonoids ambayo huweza kusaidia kushusha presha.

5. Matumizi ya shayiri(Oat)

Shayiri ina beta-glucan ambayo huweza kusaidia kama una tatizo la Presha.

6. Kula mboga za majani ambazo ni Leafy green vegetables kama vile;

  • Cabbage,
  • Spinach n.k

7. Matumizi ya vitunguu saumu(garlic),

Pia Vitunguu saumu ni msaada mzuri kwa mtu mwenye Presha ya Kupanda.

8. Kula vyakula jamii ya Samaki hasa oily Fish

9. Matumizi ya nyanya, Watu wengi hawafahamu kwamba nyanya ina Lycopene ambayo ni Msaada sana kwa mtu mwenye Presha ya kupanda

10. Matumizi ya vitu kama vile Walnuts, Pamoja na baadhi ya Spices(Viungo).

Bonus tips; Epuka Vitu hivi kama una presha ya kupanda;

  • Matumizi ya chumvi nyingi
  • Matumizi ya vitu vyenye caffeine
  • Unywaji wa Pombe N.k

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!