Vyakula Vinavyopunguza Kichefuchefu Kwa Wajawazito

VYAKULA VINAVYOPUNGUZA KICHEFUCHEFU KWA WAJAWAZITO(Morning sickness)

Mwanamke hupatwa na mabadiliko mengi sana mwilini Wakati wa ujauzito ikiwa ni pamoja na hili la kupatwa na kichefuchefu cha mara kwa mara pamoja na kutapika, yote hii ni kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini ambayo hutokea kipindi cha ujauzito hasa kwenye miezi mitatu(3) ya kwanza yaani First Trimester.

Zipo makala mbali mbali ambazo zinasaidia kutoa maelekezo kuhusu njia mbali mbali za kupunguza tatizo la kichefuchefu pamoja na kutapika kwa mama mjamzito,ila katika makala hii tutadeal zaidi na aina ya vyakula vya kukusaidia kupunguza tatizo la kichefuchefu pamoja na kutapika wakati wa ujauzito.

Mbali na aina ya vyakula vya kupunguza tatizo la kichefuchefu pamoja na kutapika,mama mjamzito hushauriwa kula kidogo kidogo ila mara nyingi zaidi na kuepuka kula chakula kingi kwa wakati mmoja,hii itamsaidia sana kupunguza tatizo hili la kupata kichefuchefu na kutapika,lakini pia kupata nguvu ya kutosha kutokana na kula chakula.

VYAKULA VINAVYOPUNGUZA KICHEFUCHEFU KWA WAJAWAZITO(Morning sickness) NI PAMOJA NA;

1. Matumizi ya viazi, Chumvi pamoja na wanga uliopo kwenye viazi huweza kusaidia kupunguza mate mdomoni ambayo ndyo chanzo kikubwa cha kichefuchefu na kusaidia kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu

ANGALIZO; matumizi ya viazi kwa kiasi kikubwa huweza kukusababishia matatizo mengine kama vile; kuongeza tatizo la kiungulia n.k

2. Matumizi ya Limao, Unaweza kukamua limao kwenye maji au kunusa maganda yake,vyote hivi kwa pamoja huweza kupunguza tatizo la kichefuchefu pamoja na kutapika kwa kiasi kikubwa.

3. Matumizi ya vidonge vya Folic acid au FEFOL ambavyo mama mjamzito hupewa wakati anahudhuria kliniki,mbali na kusaidia kuongeza damu,kupunguza matatizo ya kuzaliwa kwa watoto wenye tatizo la mgongo wazi pamoja na vichwa vikubwa,Pia vidonge hivi huweza kusaidia kuongeza madini ya chuma na kuondoa tatizo la mama mjamzito kula udongo pamoja na tatizo la kichefuchefu

4. Epuka kula vyakula venye viungo vingi ndani yake pamoja na Mafuta mengi,badala yake pendelea kula vyakula vyenye Vitamins kama vile Vitamin B6 pamoja na Proteins.

5. Pia kuna pipi maarufu kama Preggie Pops,pipi hizi huweza kumsaidia mama mjamzito kupunguza tatizo la kichefuchefu pamoja na kutapika

6. Unashauriwa kuendelea kunywa maji ya kutosha kwa siku angalau lita 2.5 mpaka 3, kwani wakina mama wengi wajawazito hupatwa na tatizo la kupungukiwa na maji ya mwili,choo kigumu yaani constipation n.k

7. Epuka kula chakula pamoja na kinywaji chochote hasa vinywaji vyenye sukari nyingi kwa wakati mmoja,angalau vipishane kati ya chakula na kinywaji kwa muda wa nusu saa au dakika 30 kabla au baada.

8. Unashauriwa kabla ya kutoka kitandani pata kifungua kinywa chochote pamoja na vitafunio vikavu,mkate mkavu n.k, hivi vitakusaidia pia kupunguza tatizo la kichefuchefu pamoja na kutapika hasa wakati unaamka asubuhi

9. Matumizi ya Tangawizi pia husaidia kupunguza tatizo la kichefuchefu pamoja na kutapika

ANGALIZO: Tumia kwa kiwango kidogo, weka ndani ya chai n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!