Ticker

6/recent/ticker-posts

Watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi hakikisha mnafuata haya



Watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi hakikisha mnafuata haya

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI) Profesa Said Aboud amewahimiza watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi kuhakikisha wanafuata maelekezo ya daktari ili kuepukana na tatizo la usugu.

Prof Aboud ametoa ushauri huo leo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Kongamano la Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa lililofanyika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) ambapo amesema kwa mtumiaji wa dawa kiholela na asiyefuata maelekezo ya daktari husababisha kirusi cha ukimwi kujenga usugu.

“Mgonjwa anatakiwa kutumia dozi ya dawa kwa makini kwa kuzingatia maelekezo. Akitumia kiholela yule mdudu kirusi cha ukimwi anapata fursa ya kujenga usugu dhidi ya ile dawa anayotumia na matokeo yake ni kushindwa kufanya kazi,”amesema.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo wa Muhas, Profesa  Emmanuel Baladya amesema kongamano hilo ni mwendelezo wa juhudi zao kuhakikisha wanashirikisha wadau mbalimbali kutoka wizara ya afya na sehemu nyingine kuangalia ni wapi wamefika katika kushughulikia tatizo hilo.

Kwa mujibu wa Profesa Baladya, karibu asilimia tano ya wanaotumia baadhi ya dawa wana usugu ambapo pia, wapo wanaotumia dawa haziwasaidii na asilimia 90 wamegundulika wana usugu.

Mhadhiri Mwandamizi na Mtafiti wa  Muhas,  Dk Doreen Kamori amesema mwaka 2020 walifanya utafiti mikoa 22 kuangalia ukubwa wa tatizo la usugu wa dawa za kufubaza na kupunguza makali ya VVU na kugundua wenye usugu wengi ni wale walioko kwenye matibabu.

Amesema dawa mojawapo inayojulikana duniani kuwa ni nzuri sana  iliyoingizwa nchini 2019  ya dolutegravier licha ya kusifiwa kwa ubora na ufanisi wake wa kupunguza makali wamegundua ina  viashiria vya kuonesha kuna resistance dhidi ya dawa hiyo.

Dk Kamori amesema wamegundua  kuna watu asilimia 5.8 dawa hiyo ilishindwa kufanya kazi vizuri.w

“Tunaona kama nchi tunapofikiria kubadilisha dawa au kuitambulisha katika nchi ni vyema kuweka miongozo na kujiandaa vizuri kwa kufanya tafiti kuangalia wingi wa virusi kwa watu walioko kwenye tiba na kujipanga taratibu kuingia kwenye dawa mpya, kuwafuatilia watu wanaoishi na virusi kubaini kama zina changamoto,”amesema.



Post a Comment

0 Comments