Ticker

6/recent/ticker-posts

WHO: Mtu mmoja hufa kwa kuumwa na nyoka kila baada ya dakika nne hadi sita



WHO: Mtu mmoja hufa kutokana na kuumwa na nyoka kila baada ya dakika nne hadi sita

Shirika la Afya Duniani (WHO) siku ya Jumanne lilisema kuwa mtu mmoja hufa kutokana na kuumwa na nyoka kila baada ya dakika nne hadi sita, na zaidi ya theluthi moja ya waathiriwa wote wana umri wa chini ya miaka 20.

“Wakati nyoka wenye sumu husambaa kwa upana katika maeneo ya dunia ya kitropiki na baridi, na hatari kubwa zaidi kwa afya ya umma hutokea katika mataifa ya kipato cha chini na cha kati ‘ David Williams, mtaalamu wa WHO kuhusu nyoka na kuumwa na nyoka, aliambia mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

Matamshi yake yalikuja kabla ya Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji kuhusu Kuumwa na Nyoka, ambayo huadhimishwa kila Septemba 19.

Kulingana na mtaalamu huyo, visa milioni 1.8-2.7 vya kuumwa na nyoka hutokea kila mwaka, na hivyo kusababisha vifo kati ya 81,000-138,000.

Wengi wa kuumwa na nyoka hutokea Asia, Afrika, Marekani Kusini, Williams alisema, wakati inakadiriwa watu milioni 1.2 walikufa kutokana na kuumwa na nyoka nchini India pekee mwaka 2000-2019 – wastani wa 58,000 kila mwaka.

Alisisitiza kuwa si kila mtu anayeumwa na nyoka husababisha vifo, lakini kwa kila anayefariki dunia, watatu zaidi hubaki na “ulemavu wa muda mrefu au wa kudumu” mfano kovu la mwili kudhoofika au hata kukatwa viungo.

Akizungumzia tishio hili, alisema maeneo yaliyoathiriwa zaidi na kuumwa na nyoka hayana uwezo wa kupata matibabu ya kutosha.

Makala Zaidi,Fahamu Kuhusu Kuumwa na Nyoka

KUUMWA NA NYOKA:

janga hili linazikumba jamii nyingi zilizo kwenye maeneo ya joto kote duniani.  Takribani visa milioni 1.8-2.7 vya kuumwa na nyoka hutokea kila mwaka, na hivyo kusababisha vifo kati ya 81,000-138,000.

WATU WALIOKATIKA HATARI

1. Wavuvi

2. Wawindaji

3. Wakulima vijijini

4. Watoto wadogo

5. Watu wanaoishi kwenye mazingira/nyumba duni na wasio na elimu ya kujikinga na wasio na huduma za afya katika maeneo yao. 

Nyoka wenye sumu huweza kugawanywa kwenye makundi makuu mawili nayo kitaalamu ni 

1. Crotalinae

2. Elapidae

Hii ni kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika hasa marekani. 

Tofauti za makundi haya ni, 

1. Crotalinae

Nyoka hawa sifa zao ni

- wana vichwa vya pembe tatu

- mboni za macho yao huwa mfano wa mviringo husio sawa

- wanavishimo joto usoni

- wana chonge/meno makubwa mfano wa msitatili kwa mbele. 

2. Elapidae

Nyoka hawa sifa zao ni

- wana vichwa vya duara

- mboni zao ni za mviringo

- hawana chonge

- wamegawanyika katika makundi makuu matatu. 

Ajari za kuumwa na nyoka hasa miguuni ni nyingi sana. 

NINI HUTOKEA UUMWAPO NA NYOKA

Nyoka katika kundi la crotalinae huweka sumu zao chini ya ngozi ya binadamu wamuumapo yaani katika ukanda/tishu wa mafuta.  Mara chache sumu huweza fika kwenye misuli na hivyo kupelekea kufa kwa seli na kuoza kwa eneo ilo na hata shida katika mfumo wa mzunguko wa damu. Sumu hizi zinamadhara katika damu. 

Iwapo sumu itapelekea kuharibika na kuvuja kwa mishipa midogo ya damu, hali hii huweza kupelekea kukusanyika kwa majimaji ktk mapafu na mfumo mzima wa upumuaji, shinikizo la chini la damu nk. Pia sumu hizi zinaweza pelekea kuharibika kwa mfumo mzima wa ugandaji wa damu na hivyo kupelekea kutokwa na damu nyingi. 

Sumu hizi zina vijenzi vya protini amino asidi,  mafuta wanga na madini mbalimbali yakiwemo zinc. Protein hizi hupelekea kuharibika kwa ukuta ulindao seli,  viunganishi vya seli na hivyo kuleta madhara makubwa mwilini. Madhara yanategemea wingi/kiwango na ubora wa sumu yenyewe. 

Sumu za elapidae zinavijenzi ambavyo hushambulia mfumo mzima wa fahamu na hivyo kusababisha madhara makubwa ndani ya muda mfupi ikiwemo kushindwa kupumua. 

KUUMWA NA NYOKA,DALILI ZAKE

crotalinae husababisha

1. Kuvimba

2. Maumivu makali mfanano wa kuungua na moto

3. Kuvilia damu

4. Malengelenge

5. Iwapo matibabu yatachelewa hupelekea kuoza kwa eneo husika

Dalili nyingine ni

6. Kichefu chefu na kutapika

7. Shida katika kuona

8. Ladha ya chuma mdomoni

9. Kukakamaa kwa misuli

Elapidae husababisha

1. Kushindwa kupumua

2. Kushindwa kufanya kazi kwa milango ya fahamu

3. Kupooza kwa sehemu mbalimbali za mwili

NINI KIFANYIKE BAADA YA KUUMWA NA NYOKA. 

Ziko njia mbalimbali za asili/ tiba mbadala ambazo zimekuwa zikitumika. Baadhi ya njia hizi zinapingwa kitaalamu na badhi zinafanyiwa uchunguzi.  Njia kama kuchana chana kidonda,  kuweka manyoya ya ndege au kutumia denge,  kunyonya sumu,  kufunga kamba na nyinginezo zimeonekana kuwa na madhara zaidi ya faida hivyo zinapingwa na wataalamu. 

Iwapo mtu ameumwa na nyoka haraka fanya yafuatayo. 

1. Toka/ mtoe eneo ambapo tukio imetokea

2. Ondoa kitu chochote kinachobana eneo hilo kuzuia madhara iwapo uvimbe utatokea.  Tambua nyoka wengi wenye sumu hawasababishi vifo. 

3. Epuka kutumia njia za asili 

4. Safisha kidonda kisha nyanyua eneo husika juu ya usawa wa moyo na kisha haraka muwaishe hospitali. Huko matibabu yatafanyika kama inavyostahiri. 



Post a Comment

0 Comments