Dalili za Upungufu wa vitamin d,soma hapa kufahamu
Katika makala hii tunazungumzia tatizo la upungufu wa vitamin D mwilini yaani kwa kitaalam Vitamin D deficiency,
Kwa ujumla, vitamin mbali mbali ni muhimu sana kwenye mwili wako na kila aina ya vitamin ina kazi zake mwilini, hapa nazungumzia mfano;
- vitamin A,
- Vitamin B6,
- Vitamin C,
- Vitamin D,
- Vitamin B9,
- Vitamin B12 n.k
Upungufu wa vitamin D mwilini unasababishwa na nini? Na dalili zake ni zipi?(soma makala hii)
CHANZO CHA UPUNGUFU WA VITAMIN D MWILINI NI PAMOJA NA;
- Kula vyakula ambavyo havina vitamin D kwa muda mwingi
- Kukaa mbali na jua kwa muda mrefu kwani utengenezaji wa vitamin D mwilini mwako hutegemea pia jua.
- Figo zako kushindwa kubadilisha vitamin D kuwa katika hali ya kutumika zaidi hasa kwa watu wenye umri mkubwa
- Kuwa na ngozi nyeusi sana, tafiti zinaonyesha melanini huweza kupunguza ngozi kutengeza vitamin D pale inapopigwa na jua
- Tatizo la mfumo wako wa umeng'enyaji kushindwa kufyoza vizuri vitamin D mbali na chakula unachokula chenye vitamin vya kutosha.
DALILI ZA UPUNGUFU WA VITAMIN D MWILINI
Dalili za upungufu wa vitamin d ni pamoja na;
- Kupata maumivu ya mgongo mara kwa mara
- Kupata maumivu ya misuli,joint pamoja mifupa ya mwili mara kwa mara
- Kuwa na tatizo la vidonda kutokupona haraka
- Uchovu wa mwili kupita kiasi
- kuwa na tatizo la Nywele kukatika sana na kunyonyoka zenyewe
- Watoto kuwa na shida ya matege
- Kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara kutokana na kinga yako ya mwili kutokufanya kazi vizuri
N.k
TIBA YA UPUNGUFU WA VITAMIN D MWILINI
- Matibabu ya upungufu wa vitamin D mwilini huhusisha matumizi ya vyakula vyenye kiwango cha kutosha cha vitamin D, Dawa zakusaidia umeng'enyaji pamoja na ufyozwaji wa vitamin D mwilini, pamoja na matumizi ya Virutubisho mbali mbali yaani supplements
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!