Kitandani kuna mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusi
Kitandani kuna mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusi
Fahamu kwamba kitanda chako kinaweza kuwa na mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusi. Ingawa Kila mmoja wetu anadhani kitanda chake ni mahali pazuri sana pa kukaa, ndyo ni Sahihi lakini je unajua pia unaweza kupata vimelea wengi wa magonjwa kitandani?
Kitandani kuna joto ambalo linaweza kutengeneza mazingira mazuri kwa Vimelea wa magonjwa kukua, pamejaa jasho, mate, chembechembe za ngozi zilizokufa na ndio chakula kwa ajili ya vimelea hao.
Mfano, vijidudu vidogo sana vinavyoishi kwenye vumbi. Tunamwaga seli za ngozi milioni 500 kwa siku, vijidudu hivyo hula seli hizo. Kwa bahati mbaya, vidudu hivyo na mabaki yake (kinyesi) vinaweza kusababisha mzio, pumu pamoja na tatizo la ukurutu.
Mashuka ya kitanda ni kimbilio la bakteria pia. Mwaka 2013, watafiti katika Taasisi ya Pasteur de Lille huko Ufaransa walichunguza mashuka ya kitanda cha hospitali na kugundua yamejaa bakteria wa Staphylococcus, ambao hupatikana zaidi kwenye ngozi ya binadamu.
Ingawa spishi nyingi za staphylococcus hazina madhara, lakini baadhi, kama vile S. aureus, wanaweza kusababisha maambukizi ya ngozi, chunusi na hata nimonia kwa wagonjwa walio na kinga dhaifu.
"Watu hubeba bakteria wengi katika ngozi zao," anasema Manal Mohammed, mwanabiolojia wa Chuo Kikuu cha Westminster nchini Uingereza.
"Ingawa bakteria hawa kwa kawaida hawana madhara, ila wanaweza kusababisha ugonjwa mbaya ikiwa wataingia mwilini kupitia majeraha ya wazi, ambayo ni ya kawaida hospitalini," anasema Manal.
Vitanda vya hospitali
Mwaka 2018, wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Ibadan nchini Nigeria walipata bakteria wa E. koli katika mashuka ya kitanda cha hospitali ambayo hayajafuliwa, pamoja na bakteria wengine wa pathogenic wanaojulikana kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo, nimonia, kuhara, homa ya uti wa mgongo na sumu katika damu.
Mwaka 2022, watafiti walikusanya sampuli kutoka kwenye vyumba vya wagonjwa waliolazwa hospitalini kwa ugonjwa wa mpox. Waligundua kuwa kitendo cha kubadilisha shuka la kitanda hutoa chembe za virusi kwenye hewa.
Mwaka 2018, mfanyakazi wa afya wa Uingereza inaaminika alipata ugonjwa huo baada ya kuambukizwa virusi wakati akibadilisha mashuka ya kitanda cha mgonjwa.
"Mashuka ya hospitalini huoshwa kwenye maji makali ya moto, ambayo huua bakteria wengi," anasema David Denning, profesa wa magonjwa ya kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza.
Isipokuwa bakteria wa C. difficile, ambaye husababisha kuhara, hasa kwa watu wazee. Kuosha kunaweza kuharibu nusu ya bakteria C. difficile, lakini seli za bakteria hao ni vigumu kufa. Hata hivyo, viwango vya maambukizi ya C. difficile vimepungua nchini Uingereza.
Bila shaka, kuna uwezekano mkubwa wa kupata bakteria wa pathogenic katika kitanda cha hospitali ambapo mgonjwa amelala kuliko katika kitanda cha mtu mwenye afya.
Vitanda vya Nyumbani
Mwaka 2013, kampuni ya vitanda ya Marekani ya Amerisleep ilichukua sampuli kutoka katika foronya ambayo haikuwa imeoshwa kwa wiki moja. IIikuwa na takribani bakteria milioni tatu kwa kila nchi ya mraba - takribani mara 17,000 zaidi ya bakteria waliopo kwenye sinki la choo.
Mwaka 2006, Denning na wenzake walikusanya mito sita kutoka kwa marafiki na familia. Mito hiyo ilikuwa ikitumika mara kwa mara na ilikuwa na umri wa kati ya miezi 18 na miaka 20. Mito yote ilikuwa na fangasi, hasa aina ya Aspergillus fumigatus - ambao hupatikana kwa wingi kwenye udongo.
"Unazungumza mabilioni au matrilioni ya chembe za fangasi kwenye kila mto," anasema Denning.
"Chanzo cha kupatikana fangasi wengi ni kwa sababu wengi wetu tunatokwa na jasho usiku. Pia sote tuna wadudu wa vumbi vitandani mwetu, na kinyesi cha wadudu hao hutoa chakula kwa fangasi. Na kisha jioni mto hupata joto kwa sababu kichwa chako hulala hapo, kwa hivyo kuna unyevu, kuna chakula, na kuna joto.”
Kwa kuwa wengi wetu huwa hatuoshi mito yetu, fangasi huishi katika hali ya utulivu na wanaweza kuishi kwa miaka. Hata kama utaosha foronya, fangasi wanaweza kuishi katika halijoto ya hadi nyuzi joto 50C (122F), na kwa vyovyote vile kuosha mito au foronya kunaweza kuifanya iwe na unyevu zaidi, na hivyo kuruhusu kukua zaidi.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!