Kupata mafua baada ya tendo la ndoa,chanzo na Tiba
Mwanaume kupata Tatizo la kupata Mafua baada ya tendo la ndoa husababishwa na nini?
Post-orgasmic illness syndrome (POIS) ni hali adimu ambayo huwaathiri wanaume, hali hii huambatana na dalili mbali mbali ambazo hujitokeza mara tu baada ya mwanaume kumwaga(ejaculation), Dalili hizo ni pamoja na;
- Mwili Kuchoka sana kupita kiasi
- Kupata hali kama ya Mafua
- Pua kuziba
- Kuhisi hali ya kuungua Machoni pamoja na macho kuwasha
- Kupata shida ya kuzingatia(concentration difficulties),
- Mwili kutokutulia,
- Mwili kuwasha
- Kukosa mudi au kuwa na hali ya huzuni n.k
Chanzo cha Kupata mafua baada ya tendo la ndoa
Kama tulivyosema hapo awali, dalili hii ya kupata Mafua baada ya tendo la ndoa husababishwa na tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Post-orgasmic illness syndrome (POIS).
Katika nakala ya mapitio ya hivi majuzi iliyochapishwa katika Jarida la Kimataifa la Utafiti wa Impotence, watafiti walichambua kuhusu hali hii ya post-orgasmic illness syndrome (POIS), hali adimu ambayo haijulikani sana.
Dalili za Post-Orgasmic illness syndrome(POIS)
POIS huhusishwa na dalili mbali mbali kama vile kuziba kwa pua, kuwa na Mafua,macho kuwasha, na uchovu mwingi, unaotokea baada ya kujamiiana, kumwaga manii kwa hiari, na kupiga punyeto. Dalili hizi zinaweza kuonekana ndani ya muda mfupi baada ya kumwaga lakini kwa ujumla ndani ya dakika 45 na zinaweza kudumu kwa siku nzima au zinaweza kuisha ndani ya siku saba.
Hali hii ikitokea kwa mara ya kwanza kipindi cha balehe hujulikana kama Primary POIS, Lakini ikitokea baadae huitwa Secondary POIS. Na tafiti huonyesha asilimia 14-49% ya Wanaume hupata primary POIS.
Kwa hiyo, hii ndyo Sababu kubwa ya Tatizo la kupata Mafua baada ya tendo la ndoa Kwa Mwanaume.
Zipo Dalili kuu Tisa(9) ambazo huonyesha hali hii ya POIS, ambapo ni dalili na Ishara ambazo huanza kujitokeza baada ya Tendo la ndoa, dalili hizo ni pamoja na:
- Kuwa na Upele kwenye ngozi pamoja na muwasho baada ya tendo
- Kuhisi hali ya koo kuuma,throat symptoms,
- Kupata maumivu ya kichwa
- Kupata shida ya kuzingatia, poor concentration,
- Mwili kuchoka sana
- Macho kuwasha
- Kupata Mafua,Pua kuziba n.k
- Kupata tatizo la myalgia, Irritation n.k
- Kupata Homa
Chanzo cha Post-orgasmic illness syndrome (POIS)
Mpaka Sasa chanzo halisi cha POIS hakifahamiki, lakini watafiti wametoa nadharia kwamba inaweza kuwa na msingi wa kinga ya mwili unaohusisha hypersensitivity kwa maji ya semen. Upimaji mzuri ulipata ushahidi wa hypersensitivity, lakini viwango vya immunoglobulin E (IgE) vilibakia bila kubadilika.
Nadharia nyingine ni kuhusu hali ya autoimmune ambapo seli zinazowasilisha antijeni za urethra huchochea uanzishaji wa T-cells zinapotambua peptidi kwenye shahawa. Hali kama hiyo kwa wanawake inaweza kuhusisha tishu kwenye eneo la uke.
Ukosefu wa udhibiti wa mfumo wa neva pia umehusishwa na tatizo la POIS,
Kukosekana kwa usawa wa homoni(hormone imbalance) pia kunaweza kuwa sababu, Mfano; uchunguzi mmoja uligundua kuwa kutoa progesterone kwa Mwanaume mwenye tatizo hili kulitatua dalili hizi.
Matibabu ya Tatizo la Kupata mafua baada ya tendo la ndoa
Matibabu Pekee ya Hali hii hutegemea na chanzo husika, Mfano kama shida ipo kwenye vichocheo vya mwili,basi tiba itakuwa kwenye vichocheo hivi n.k
lakini ikiwa una tatizo hili na hujapata Tiba bado;
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Journal reference:
Post orgasmic illness syndrome: a review. Odusanya, B.O., Pearce, I., Modgil, V. International Journal of Impotence Research (2024). DOI: 10.1038/s41443-024-00860-3, https://www.nature.com/articles/s41443-024-00860-3