Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito
Baadhi ya Watu hujiuliza,yapi ni Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito? Watu wengi wanajiuliza kufanya Mapenzi Mwanamke akiwa mjamzito je ni salama au kuna Madhara?
Kwa kuliona hilo na baada ya kupata Maswali mengi,Leo katika Makala hii tumechambua kuhusu Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito Pamoja na Vitu vya Kuzingatia Zaidi kwenye kipindi hiki cha Ujauzito.
Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito
Je ni Sawa kufanya Mapenzi wakati wa ujauzito?
Unachotakiwa kufahamu ni kwamba,Mtoto ambaye anakua tumboni(fetus) hulindwa na kufunikwa na maji ya Uzazi-amniotic fluid, Pamoja na misuli imara kabsa ya mfuko wa uzazi wenyewe,
Hii inamfanya mtoto kukua kwenye Mazingira Salama zaidi akiwa ndani ya tumbo la Uzazi bila kujali unafanya mapenzi au hufanyi.
Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito
• Hakuna Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito kama mama huyu hana historia ya matatizo yoyote ya kiafya(complications)
• Sio salama kwa Mama mjamzito kufanya Mapenzi kama akiwa na historia ya matatizo ya kiafya kama vile;
- Kupata uchungu mapema kabla ya wakati(preterm labor)
- Matatizo kwenye kondo la nyuma au placenta problems
- Kuvuja damu Ukeni kupita kiasi
- Kutokwa na maji ya Uzazi yaani amniotic fluid
- Mlango wa uzazi(Cervix) kuanza kufunguka kabla ya wakati au kuwa na tatizo la cervical incompetence
- Kuwa na tatizo la kondo la nyuma(placenta) kushuka na kufunika mlango wa uzazi kwa kitaalam hujulikana kama placenta previa n.k
Kama una matatizo kama haya unashauriwa kuomba Msaada na Ushauri wa wataalam wa afya kuhusu Njia Salama za kutunza Ujauzito wako ili kukusaidia kuzuia Madhara wakati wa ujauzito,kisha kujifungua Salama.
Kumbuka: Kufanya Mapenzi wakati wa Ujauzito hakusababishi mimba kutoka yenyewe(miscarriage),Ingawa kama una shida hii pia, ni vizuri kuchukua tahadhari.
• Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito ni Pamoja na kuongeza hatari ya kupata magonjwa mbali mbali,
Ikiwa huchukui tahadhari zozote za kujikinga na magonjwa mbali mbali ikiwemo magonjwa ya Zinaa, kufanya Mapenzi kwenye kipindi hiki kunaweza kuongeza hatari zaidi ya wewe kupata magonjwa mbali mbali.
Kutokana na mabadiliko ya vichocheo mwilini, pamoja kushuka kwa kinga ya mwili kipindi cha Ujauzito,inaweza kusababisha mama mjamzito kupata magonjwa kwa urahisi,
magonjwa hayo ni pamoja na;
- Ugonjwa wa UTI
- Tatizo la fangasi Sehemu za Siri
- Tatizo la Pid
- Magonjwa mbali mbali ya Zinaa kama ugonjwa wa kaswende,kisonono,Chlamydia, kupata virusi vya human papiloma virus(HPV) n.k
Kumbuka magonjwa kama kaswende huweza kumuathiri mpaka mtoto.
FAQs; Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara
Je, kuna Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito?
• Hakuna Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito kama mama huyu hana historia ya matatizo yoyote ya kiafya(complications),
Lakini pia endapo wahusika wakichukua tahadhari zote za kujikinga na Magonjwa mbali mbali yakiwemo magonjwa ya Zinaa(Sexual transimitted diseases).
Hitimisho
Hakuna Madhara ya kufanya Mapenzi kwa Mama Mjamzito kama mama huyu hana historia ya matatizo yoyote ya kiafya(complications),
Pia hakikisha unachukua tahadhari zote za Kujikinga na magonjwa mbali mbali yakiwemo magonjwa ya Zinaa, ili wewe pamoja na mtoto tumboni muwe Salama zaidi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!