Mlipuko wa kipindupindu, surua na Mpox waathiri mamilioni Afrika

Mlipuko wa kipindupindu, surua na Mpox waathiri mamilioni ya Watu Mashariki mwa Afrika

Daktari akitoa huduma za afya katika kituo cha kutibu kipindupindu kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bulengo jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC.

Takribani watu milioni 67 wakiwemo wakimbizi na wasaka hifadhi katika  ukanda wa Mashariki mwa Afrika wanahitaji misaada ya kibinadamu.  Idadi hiyo ni zaidi ya asilimia 21 ya idadi ya watu wote duniani wenye uhitaji wa misaada ya kibinadamu.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric akizungumza na waandishi wa habari hii Jana jijini New York, Marekani amenukuu Ofisi ya  Umoja wa Mataifa  ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA ikisema kuwa ukanda huo unakabiliwa na majanga makubwa zaidi ya kibinadamu yakichochewa na mabadiliko ya tabianchi, mizozo, ukosefu wa utulivu wa kisiasa, zahma za kiuchumi na milipuko ya magonjwa.

Milipuko hiyo ya magonjwa ni pamoja na kipindupindu, surua na mpox. Hadi tarehe 26 Septemba, takribani wagonjwa 776 wa mpox walikuwa wameripotiwa kwenye ukanda huo. Na kama mnavyofahamu, virusi vya homa ya Marburg hivi sasa vinasambaa. Takribani wagonjwa 29 wamethibitishwa nchini Rwanda na vifo 9.”

Kipindupindu kimesalia kuwa hofya ya afya ya umma kwa Ethiopia, Somalia, Uganda na Tanzania. Mlipuko wa kipindupindu Ethiopia umekuwa unaendelea tangu Agosti 2022. Milipuko ya surua imeripotiwa pia Burundi, Ethiopia, Kenya, Tanzania, Uganda na Sudan Kusini ambako vifo 41 vinavyohusiana na ugonjwa huo vimeripotiwa mwaka huu.

Njaa nayo ni tishio Mashariki mwa AFrika

Kando ya magonjwa, Dujarric amesema wadau wa kibinadamu wameendelea kutoa misaada ya kibinadamu kaw mamilioni ya watu.

Taarifaya OCHA inasema kuwa baadhi ya maeneo yaliyo na njaa duniani yako Mashariki mwa Afrika ambako zaidi ya watu milioni 55 wanakabiliwa na njaa kali.

Kati ya ohao milioni 26 wako Sudan ambako baa la njaa tayari limetangazwa kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani  ya Zamzam iliyoko jimbo la Darfur Kaskazini.

Uhakika wa chakula si mzuri huko Ethiopia ilihali nchini Sudan Kusini idadi  ya awtu wanaokabiliwa na njaa yakadiriwa kuwa itaongezeka maradufu mwaka huu.

Zaidi ya watoto milioni 2.5 wenye umri wa chini ya miaka mitano wanakabiliwa na utapiamlo mkali huko Ethiopia, Burundi, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini na Uganda.

Wadau wa kibinadamu wanataka kusongesha operesheni za usaidizi kwa wahitaji, lakini OCHA inasema ombi lao la usaidizi la dola bilioni 9.3 linalotakiwa kwa mwaka huu wa 2024 limechangiwa kwa asilimia 38 tu hadi mwishoni mwa mwezi uliopita.

Via; UN.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!