Nini cha kufanya ikiwa mtu amekula chakula chenye sumu
Fahamu kwamba Habari za watu kufariki dunia kutokana na kula chakula chenye sumu kwa hivi Sasa zimeongezeka na kuibua hisia za Umma hasa katika majimbo ya kaskazini mwa Nigeria.
Katika muda wa mwezi mmoja, kulikuwa na taarifa za vifo vya watu wapatao 24 katika majimbo ya Sokoto na Zamfara, ambapo Matukio hayo yaliathiri familia tatu.
Moja ya Sababu ya Watu hao kupoteza maisha katika jimbo la Sokoto ilikuwa ni kula chakula kilichochanganywa na mihogo,
Kisha kulikuwa na watu sita kutoka kwenye nyumba moja ambao walikufa baada ya kunywa supu.
Waliofariki ni pamoja na mke wa nyumba hiyo na watoto wake watano.
Katika tukio linalofanana na hilo, watu 12 walikufa katika mji wa Daki Akwas katika Serikali ya Mtaa ya Anka katika Jimbo la Zamfara, baada ya kunywa supu ya majani ya lalo yenye dawa za kuua wadudu.
Watu 25 waliotoka katika nyumba mbili walikunywa supu hiyo siku ya Ijumaa, na tangu wakati huo walianza kufa mmoja baada ya mwingine.
Mkuu wa Tume ya Afya ya Umma ya Jimbo la Zamfara, Yusuf Abubakar aliiambia BBC kuwa: "Mkulima mmoja alikwenda kunyunyizia dawa ya kuua wadudu baadhi ya mimea, miongoni mwao kulikuwa na jani la lalo, ambalo hutumika katika supu ya nyumba za Wahausa.
"Alipulizia asubuhi, wakaenda mchana kutafuta mimea ya kutengeneza supu. Kisha wakaanza kutapika, kuharisha na kupata kinyesi laini. Kisha wakapelekwa hospitali."
Afisa huyo alisema baadhi ya watu walikunywa supu nyingi kuliko wengine, hivyo wengine walifia nyumbani, wengine walifia hospitali ya Anka, na wengine walilazimika kufikishwa katika Hospitali Kuu ya Taryya huko Zamfara.
Jinsi ya kutambua mtu aliyekula chakula chenye sumu
Daktari Fatima Adamu ambaye ni Daktari wa Hospitali ya Mafunzo ya Aminu iliyopo Kano alisema, “Ukweli ni kwamba hatuzitambui dalili hizo kwa macho, kwa kawaida unapofikishwa hospitalini kuna baadhi ya maswali tunauliza, pamoja na majibu tutajua ni sumu au maumivu yoyote.
Lakini alieleza baadhi ya dalili wanazoziona kwa wale waliokula sumu, dalili hizo ni pamoja na:
- Maumivu ya tumbo
- Pamoja na Homa
Kulingana na Dk Fatima, ni kuanzia wakati huu ambapo mtu anachunguzwa kuhusu alichokula na iwapo kuna wengine waliokula chakula hicho baada yake.
Dkt. Fatima aliongeza kuwa si lazima kusubiri mapovu yatoke mdomoni mwa mtu, kwa sababu kulingana na yeye, sumu pia ina rangi.
Kinachotokea katika mwili wa mtu anapokula chakula chenye sumu
Dk.Fatima alisema kuna tatizo mara baada ya sumu anayokula mtu kwenye chakula kuingia mwilini mwake.
“Mwili utatambua kuwa kuna kitu cha ajabu kimeingia, lakini pia mwili una ulinzi wake, Hivo basi mfumo wa kinga mwili utaanza mapambano dhidi ya kilichoingia, na hapa ndipo dalili mbali mbali zitaanza kujitokeza kwa mhusika.
Je, unaweza kupona baada ya kula sumu?
" Sio kila Sumu inahitaji Tiba,Baada ya siku chache unaweza kupona hata bila Tiba, Ingawa Watu wengine wanahitaji matibabu. Hii Inategemea hali ya kinga yako na nguvu ya Sumu."
Hata hivyo, haupaswi kukaa nyumbani ikiwa unaona kuwa umekula chakula chenye sumu, ni bora kwenda hospitali haraka iwezekanavyo.
"Kwa kila sumu kuna njia za kufanya, mtu anaweza kutumia njia za kutoa alichokula, na mwingine atapewa dawa, lazima azuie alichokula kisiingie kwenye damu yake, kisha atakitoa kwa njia ya choo. atapewa dawa nyingine ya homa tu.n.k”
Haupaswi kuacha kuchukua hatua nyumbani, hii itasaidia kuzuia shida kadhaa na hata vifo.
Makosa yanayofanywa wakati mtu anakula chakula chenye sumu
Dk.Fatima alisema yapo baadhi ya mambo wanayofanya watu ili kupunguza madhara ya sumu kwenye mwili wa binadamu ambayo ni makosa kisayansi na yanaweza kumdhuru mtu.
Alisema: "Kwa mfano, utasikia mtu anaambiwa toa maziwa au kitu, au utasikia mtu anaambiwa atapike." Ikiwa ni kemikali au asidi hizo, mtu akiambiwa atapike, madhara zaidi yatatokea kwake, na inaweza kusababisha mtu kupoteza maisha.
Kwa hiyo, hakuna maana ya kusubiri mambo kama hayo, mara tu dalili zinapoonekana, ni muhimu kumpeleka mtu hospitali mara moja."
Njia za kuepuka kula chakula chenye sumu
Sumu ina madhara kwa mtu inapoingia mwilini, mtu anawezaje kujizuia kula chakula chenye sumu?
kuna baadhi ya hatua muhimu za kuchukua ili kuepuka sumu kwenye chakula:
- Safisha chakula chako vizuri
- Safisha eneo la jikoni
- Hifadhi chakula mahali pazuri ambapo hakuna kitakachochafua
- Tumia maji safi
- Tumia vyombo safi vya kulia chakula
- Hifadhi chakula kwenye jokofu
- Nawa mikono yako kila wakati
- Usiweke vifaa vya sumu karibu na jikoni