Uganda yaripoti kifo cha kwanza kinachotokana na Virusi vya Homa ya nyani,Mpox

Uganda yaripoti kifo cha kwanza kinachotokana na Virusi vya Homa ya nyani,Mpox

Takriban miezi mitatu baada ya maambukizi ya hapo awali kuripotiwa nchini. Maelezo kutoka kwa wizara hiyo yanaonyesha kifo hicho kiliripotiwa Masindi kutoka kwa mtu anayeugua na virusi vya ukimwi.

Kulingana na ripoti iliyonukuliwa kutoka kwa Wizara ya Afya na vyombo vya habari nchini Uganda, Wilaya ya Masindi imesajili maambukizi matatu ya ugonjwa wa Mpox, ambao hutambulika kwa kutoka majipu yaliyojaa usaha usoni, sehemu za siri na sehemu zingine za mwili.

Akizungumza na maofisa wa afya na viongozi wa wilaya wakati wa Misheni ya Kudhibiti Mpango wa Pamoja wa Afya wa Mwaka jijini Kampala siku ya Jumatano, Dkt. Jane Ruth Aceng, Waziri wa Afya, alitoa wito wa kuanzishwa upya kwa vikundi maalum vya kupambana na Mpox, kama vile ilivyokuwa wakati wa Covid-19.

Mlipuko wa Mpox, tunaweza kudhani ni suala rahisi lakini hali halisia ni suala gumu. Mlipuko huu ambao umeathiri dunia nzima unahitaji kudhibitiwa na kukomeshwa.

Nchini Uganda, maambukizi haya yalithibitishwa tarehe 24 Julai, 2024,” alisema.

“Mlipuko unaendelea kuenea. Hadi sasa, tuna jumla ya maambukizi 153, kati ya hizo 42 zilikuwa katika wiki moja iliyopita. Katika siku chache zilizopita, idadi ya maambukizi inaongezeka kwa kasi,” aliongeza.

Dkt. Aceng alifichua kuwa wilaya 19 zimeripoti maambukizi. Ilioathirika zaidi ni Kampala yenye maambukizi 55, ikifuatiwa na Nakasongola, jumuiya ya wavuvi, ambayo ina maambukizi 35, na Wakiso yenye maambukizi 23.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!