VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME
Vipele kwenye Uume:
Vipele Kwenye Uume: Chanzo, Dalili na Matibabu
Tatizo la vipele kwenye uume ni hali inayowapata wanaume wengi duniani kote. Hali hii inaweza kuathiri sana afya ya mwili na akili ya mtu.
Kwa bahati mbaya, wanaume wengi hawajui kuhusu hali hii na wanashindwa kutafuta matibabu sahihi,
Makala hii inalenga la kutoa elimu kuhusu Tatizo la vipele kwenye uume, ikiwa ni pamoja na sababu za hali hii, dalili zake na matibabu.
Sababu za Tatizo la vipele kwenye uume:
Tatizo la vipele kwenye uume Linaweza kusababishwa na sababu mbalimbali. Sababu hizo ni pamoja na:
- Tatizo la Balanitis,kuvimba kwa kichwa cha Uume,
Hii hutokea sana kwa wanaume ambao hawajatahiriwa, kama hujafanyiwa tohara ni ngumu sana kusafisha vizuri ngozi ya chini kabsa kwenye uume,
Bacteria, jasho pamoja na seli za ngozi zilizokufa hujikusanya na kufunika eneo hili, hii huweza kupelekea miwasho,vipele,ngozi kuwa nyekundu pamoja na uchafu kutoka chini ya ngozi ya mbele ya Uume(foreskin).
- Tatizo la ngozi linalojulikana kama Contact Dermatitis, ngozi huwa nyekundu,kuwasha au kuwa na vipele
- Kuwa na Mzio au allergic reaction juu ya vitu mbali mbali ikiwemo dawa, vitu vyenye kemikali kama sabuni za kuogea,mafuta n.k
- Kuwa na tatizo la Genital Psoriasis,
- Kuwa na tatizo la Scabies
- Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Diseases (STDs) ikiwemo;
- Ugonjwa wa kaswende(Syphilis),
- Genital herpes n.k
- Mashambulizi ya Fangasi sehemu za Siri(Yeast Infection), pia huweza kusababisha miwasho pamoja na vipele.
- Maambukizi ya Bakteria au Virusi: Maambukizi ya bakteria au virusi kwenye sehemu za siri kama vile uume, yanaweza kusababisha vipele kwenye uume. Bakteria na virusi hao hupata nafasi ya kuzaliana kwenye uume na kusababisha vipele zaidi.
- Kuwa na Ngozi Kavu: Ngozi kavu kwenye uume inaweza kusababisha vipele. Hii ni kwa sababu ngozi kavu hupasuka na kuacha nafasi ya bakteria na virusi kuzaliana kwa urahisi zaidi.
- Kutumia Dawa: Baadhi ya dawa zinaweza kusababisha vipele kwenye uume. Dawa hizo ni pamoja na dawa za kulevyia, baadhi ya antibiotics, na dawa zingine zinazotumika kutibu magonjwa mbalimbali.
Dalili za Tatizo la vipele kwenye uume:
Dalili za Tatizo la vipele kwenye uume hutofautiana kulingana na sababu ya hali hii. Hata hivyo, dalili za kawaida za Tatizo hili ni pamoja na:
• Kuvimba kwa uume: Hii ni dalili ya kawaida ya Tatizo la vipele kwenye uume. Uume unakuwa mkubwa kuliko kawaida na unaweza kuuma.
• Kuwasha: Tatizo la vipele kwenye uume linaweza kusababisha kuwasha kwenye ngozi ya uume.
• Kuvimba kwa korodani:Tatizo la vipele kwenye uume linaweza kuambatana na kuvimba kwa korodani.n.k
Matibabu ya Tatizo la vipele kwenye uume:
Matibabu ya Tatizo la vipele kwenye uume hutofautiana kulingana na sababu ya hali hii. Hata hivyo, matibabu ya kawaida ni pamoja na:
Kutumia Dawa: Kwa tatizo la vipele kwenye uume linalosababishwa na maambukizi ya bakteria au virusi, daktari anaweza kuagiza dawa za kupambana na maambukizi hayo.
Dawa hizi zinaweza kuwa za kupaka kwenye uume, au kutumika kwa njia ya mdomo.n.k
Jinsi ya kuzuia Tatizo la Vipele kwenye uume:
Kuzuia Tatizo la vipele kwenye uume ni muhimu kwa afya ya uume na mwili kwa ujumla. Hatua za kuzuia hali hii ni pamoja na:
1. Kuvaa nguo za ndani safi: Kuvaa nguo za ndani safi na kubadilisha mara kwa mara ni njia moja ya kuzuia maambukizi ya bakteria na virusi.
2. Kuepuka kugusa uume bila kuosha mikono: Kuosha mikono kabla ya kugusa uume ni muhimu sana kuzuia kuenea kwa bakteria na virusi.
3. Kuepuka kushiriki ngono bila kinga au Condom: Kujikinga wakati wa kushiriki tendo la ndoa ni njia mojawapo ya kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ikiwa ni pamoja na magonjwa yanayosababisha dalili hii ya vipele kwenye uume.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Kuota vipele kwenye mashavu ya uke:
vipele kwenye mashavu ya uke huweza kusababishwa na sababu nyingi mbali mbali ikiwemo matatizo ya ngozi,maambukizi ya magonjwa n.k,
Dalili za vipele kwenye mashavu ya uke
Kwa kawaida dalili za vipele kwenye mashavu ya uke huambatana na muwasho wa mara kwa mara, na hali hii ya muwasho huzidi kuongezeka au kuwa mbaya Zaidi pale unapojikuna eneo husika.
Kwa Ujumla dalili za vipele kwenye mashavu ya uke ni pamoja na;
- Kupata muwasho au kuhisi kuungua sehemu ya upele kuota
- Kutokea kwa vipele vinavyoonekana kwa macho
- Kuwa na malengelenge au vidonda
- Ngozi kuwa na mabaka mabaka
- Kuvimba kwa ngozi
- Wengine hupata homa
vipele kwenye mashavu ya uke huweza kuambatana pia na;
– Uchafu wenye harufu mbaya kutoka ukeni
– Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa n.k
Chanzo cha vipele kwenye mashavu ya uke
Asilimia kubwa tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke ni tatizo ambalo hutibika na husababishwa na sababu za kawaida, Ingawa wakati mwingine huweza kuwa tatizo Sugu na ambalo halitibiki kulingana na chanzo chake.
Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za vipele kwenye mashavu ya uke;
1. Matatizo ya Ngozi kama vile Contact dermatitis,
Tatizo hili la ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayosababisha vipele kwenye mashavu ya uke kwa kiasi kikubwa.
Baadhi ya Tafiti za Mwaka 2014 zilionyesha Contact dermatitis huhusika na tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke kwa karibu asilimia 50% ya wanawake wenye shida hii.
2. Tatizo la kuvimba kwa Uke au mashavu ya Uke(Vaginitis au vulvovaginitis),
kwa mujibu wa vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa “the Centers for Disease Control (CDC)”, moja ya chanzo kikubwa cha tatizo hili ni maambukizi ya bacteria au fangasi.
3. Maambukizi ya Fangasi-Yeast infections (Candida),
Watu wengi wenye vipele kwenye mashavu ya uke pia hutokana na maambukizi ya fangasi sehemu za siri hasa fangasi ambao hujulikana kama Candida albicans.
4. Magonjwa ya Zinaa kama vile Trichomoniasis (trich),
Tatizo hili huweza kusababishwa na protozoan parasite na husambazwa kwa njia ya kujamiiana.
Tiba ya Trichomoniasis ni pamoja na matumizi ya antibiotics
5. Tatizo la Psoriasis
Psoriasis ni tatizo kwenye mfumo wa kinga ya mwili(autoimmune condition) ambalo matokeo yake huathiri ngozi ikiwemo ngozi ya Sehemu za Siri.
Tatizo hili huweza kuwa chanzo cha vipele kwenye mashavu ya uke au vidonda(Psoriasis lesions),
Lakini tatizo hili la Psoriasis haliwezi kuathiri sehemu ya ndani ya Uke.
6. Maambukizi ya Virusi- Molluscum contagiosum
Molluscum contagiosum ni maambukizi ya Virusi ambayo kwa asilimia kubwa hushambulia ngozi, maambukizi haya huweza kusambaa kwa njia ya kujamiiana n.k,
Moja ya dalili zake ni kusababisha upele(bumps) wenye ukubwa wa millimeters kati ya 2 mpaka 5 (mm).
7. Ugonjwa wa Scabies
Moja ya dalili kubwa za ugonjwa wa Scabies ni kusababisha vipele kwenye ngozi ambavyo huweza kuambatana na muwasho,
Hivo wanawake wenye ugonjwa wa Scabies huwezs kupata tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke.
8. Kuwa na Chawa Sehemu za Siri(Pubic lice)
Chawa Sehemu za siri(Pubic lice) ni wadudu jamii ya parasite wadogo sana ambao huweza kuathiri nywele za Sehemu za Siri na chakula chao kikubwa ni damu ya binadamu.
Unaweza kuwapata baada ya kujamiiana na mtu mwenye hawa chawa, au kupitia nguo,mashuka,taulo za kuogea n.k kutoka kwa mtu mwenye chawa.
Wadudu hawa huweza kusababisha hali ya muwasho sehemu za Siri na eneo la mashavu ya Uke kwa ujumla.
Chawa Sehemu za Siri(Pubic lice) huweza kutibiwa na dawa kama vile permethrin (Nix).
9. Maambukizi ya Genital herpes
Genital herpes husababishwa na Virusi vinavyojulikana kama herpes simplex virus, hasa hasa aina ya 2 (HSV-2).
Huu ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa yanayoenezwa kwa kiasi kikubwa, na asilimia kubwa dalili zake huchukua siku 4 mpaka 7 kuanza kuonekana toka siku ya kuambukizwa.
Dalili zake ni pamoja na kuwa na vipele, malengelenge au vidonda vyenye maumivu pamoja na kuhisi hali ya kuungua sehemu za Siri, kuzunguka uke, kwenye matako, na sehemu ya haja kubwa.
10. Ugonjwa wa Kaswende(Syphilis)
Kaswende ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na bacteria Treponema pallidum. Ugonjwa huu pia huweza kusababisha vipele kwenye mashavu ya uke au vidonda ambazo hujulikana kama chancre.
11. Tatizo la masundosundo(Genital warts)
Tatizo hili ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa ambapo chanzo chake ni maambukizi ya human papillomavirus (HPV).
Pia tatizo hili huweza kusababisha vipele kwenye mashavu ya uke.
Hizo ndyo baadhi ya Sababu za Mwanamke kupata Tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.