Zaidi ya Watu 50 Wafariki kufuatia Boti Kuzama Ziwa Kivu, Mashariki Mwa Congo
Zaidi ya Watu 50 Wafariki kufuatia Boti Kuzama Ziwa Kivu, Mashariki Mwa Congo
Watu zaidi ya 50 wamefariki dunia huku wengine wengi wakiwa hawafahamiki walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo, Alhamisi, Oktoba 3, 2024 ambapo chanzo kinatajwa kuwa ni boti hiyo kuelemewa na mizigo pamoja na abiria waliokuwa wengi kuliko uwezo wake.
Picha zinasambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, zikionesha vikosi vya uokoaji vikijaribu kuokoa maisha ya watu wengi walioopolewa kwenye mto huo, huku video nyingine ikidaiwa kuwa ndivo jinsi boti hiyo ilivyozama.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa takribani watu 10 wameokolewa wakiwa hai na kukimbizwa hospitali.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!