Dalili za magonjwa hatari sehemu za siri

Dalili za magonjwa hatari sehemu za siri

Dalili za magonjwa hatari sehemu za siri zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa. Hapa kuna dalili ambazo hujitokeza Zaidi zinazoweza kuonyesha uwepo wa magonjwa ya zinaa au maambukizi mengine sehemu za siri:

1. Vidonda pamoja na Maumivu

Vidonda visivyo vya kawaida sehemu za siri, mdomoni, au kwenye njia ya haja kubwa huweza kuwa Ishara ya magonjwa.

Kupata Maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa huweza kuwa kiashiria kingine cha magonjwa haya.

2. Kutokwa na Uchafu Sehemu Za Siri

Kutokwa na Uchafu au majimaji yenye harufu mbaya au rangi isiyo ya kawaida (kama kijani, njano, au kahawia).

Kutokwa na damu isiyo ya kawaida (kwa wanawake) ambayo haiko kwenye kipindi cha hedhi.

Kutokwa na maji maji au Usaha Kwenye Uume n.k, Zote hizi huweza kuwa dalili za magonjwa ya Zinaa Sehemu Za Siri.

3. Kuwa na Uvimbe au Malengelenge

Malengelenge yanayojitokeza kama vipele vidogo vinavyoweza kupasuka na kusababisha vidonda.

Uvimbaji wa tezi za kinena (lymph nodes) karibu na sehemu za siri.

Vyote hivi huweza kuwa dalili za magonjwa sehemu za Siri.

4. Maumivu ya Tumbo

Maumivu ya chini ya tumbo, hasa kwa wanawake, yanaweza kuashiria maambukizi kwenye mfumo wa uzazi kama PID (Pelvic Inflammatory Disease).n.k.

5. Kuwashwa na Kubadilika kwa Ngozi

Kuwashwa au kuhisi hali ya kuungua sehemu za siri.

Mabadiliko ya rangi au uwepo wa vipele sehemu hizo, hizi pia huweza kuwa dalili za baadhi ya magonjwa Sehemu za Siri.

6. Kupata Homa

Kupata homa,Kutoa jasho sana usiku au kujisikia mchovu kupita kiasi. Huweza kuwa Dalili za uwepo wa maambukizi mwilini mwako.

Magonjwa Hatari Yanayoweza Kusababisha Dalili Hizi:

Kwa Ujumla Baadhi ya Magonjwa ambayo huweza Kusababisha dalili hizi ni pamoja na;

  • Kaswende (Syphilis): Mfano vipele au Vidonda visivyo na maumivu katika hatua ya awali
  • Kisonono (Gonorrhea): Maumivu wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu mzito, Usaha n.k
  • Klamidia (Chlamydia): Mara nyingi haina dalili mwanzoni lakini baadae zinaweza kuonekana
  • Herpes Simplex Virus (HSV): Malengelenge au vidonda vinavyojirudia mara kwa mara
  • Virusi vinavyojulikana kama Human Papillomavirus (HPV): Vinaweza kusababisha masundosundo(warts),Vipele au vinundu, vingine husababisha saratani ya kizazi au sehemu za siri.
  • Ukimwi (HIV/AIDS): Dalili za upungufu wa kinga ya mwili pamoja na magonjwa nyemelezi huweza kujitokeza pia

Unapaswa Kufanya Nini?

Tafuta Matibabu Haraka: Unapoona dalili yoyote isiyo ya kawaida, hakikisha unakutana na wataalam wa afya kwa Msaada wa haraka, au Kwa Ushauri zaidi,Elimu na Tiba tuwasiliane hapa hapa ndani ya afyaclass,kupitia kwenye namba +255758286584.

Epuka Kujitibu Bila Ushauri wa Daktari: Tiba isiyo sahihi inaweza kuzidisha tatizo.

Zuia Maambukizi: Tumia kinga kama kondomu, kuwa mwaminifu kwa mwenza mmoja, au punguza idadi ya wapenzi.n.k.

Ukiona dalili yoyote, usisite kutafuta ushauri wa kitaalamu kwa sababu magonjwa haya yanaweza kusababisha madhara makubwa ikiwa hayatatibiwa kwa wakati.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!