Kutokwa na uchafu wa njano ukeni,chanzo na Tiba

Kutokwa na uchafu wa njano ukeni,chanzo na Tiba

Si kila Wakati kutokwa na Uchafu wa Njano ukeni ni tatizo,


Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni wakati mwingine inaweza kuwa ishara kwamba hedhi yako inakuja au kuashiria ujauzito katika hatua za mwanzo kabsa.  Pia hali hii inaweza kutokea kutokana na kazi za asili za Ukeni. 

KUMBUKA; Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni ni kawaida ikiwa Uchafu huo ni mweupe, mwepesi, na hauna harufu yoyote. Ingawa pia unaweza kuanza kutoka ukiwa mzito na kubadilika kuwa mwepesi kadri siku zinavyoenda. Pia unaweza kuwa na rangi ya manjano nyepesi na bado ukuwa wa kawaida kabisa.


Kwanini Aina hii ya Uchafu huweza kutoka Ukeni ukiwa karibu na Period yako au Ukiwa na Mimba?

Kipindi cha Hedhi;

Kutokwa na uchafu ukeni kunaweza kubadilika kutokana na mabadiliko ya homoni. Katika sehemu ya katikati ya mzunguko wako wa hedhi, ujazo wa majimaji ya ukeni utaongezeka na kuwa mithili ya Ute kama wa yai.  Hata hivyo, uchafu huo unapogusana na hewa, unaweza kupitia mchakato unaoitwa oxidation unaosababisha kugeuka rangi ya krimu, mawingu au njano hafifu, Rangi hizi zote ni za kawaida kabisa. 

Kipindi cha Mwanzo wa Ujauzito;

Kuongezeka kwa Uchafu kutoka ukeni inaweza kuwa ishara ya mapema ya ujauzito.  Wakati wa ujauzito, mwili hujiandaa kwa kulainisha shingo ya kizazi au Cervix pamoja na kuta za uke.  Ili kuzuia maambukizo kufika kwenye uterasi, mwili hutoa uchafu mwingi zaidi.

 Utoaji huu wa Uchafu ni wa kawaida na Mara nyingi huwa na rangi nyeupe.  Hata hivyo, Unaweza pia kugeuka kuwa njano unapogusana na hewa, kama vile unapobakia katika nguo ya ndani kwa muda mrefu.

Kutokwa na Uchafu wa Njano Ukeni kama kiashiria cha Ugonjwa

Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni kunaweza kuonyesha kuwa una maambukizi ya magonjwa ya zinaa-Sexual transimmited diseases (STDs) au hali zingine zinazohitaji matibabu.  Hii ni kweli hasa ikiwa Uchafu huu unatoka ukiwa na rangi nyeusi,kijani kibichi, au njano pamoja na harufu mbaya.

 Ni muhimu kuonana na mhudumu wa afya kwa kutokwa na uchafu wowote usio wa kawaida ukeni.  Mbali na kuwa ishara kwamba unaweza kuhitaji huduma ya matibabu, unaweza kuwa katika hatari ya kupitisha maambukizi kwa mpenzi wako ikiwa mtafanya tendo, na hivo nyinyi wawili mnaweza kuhitaji matibabu.


Uchafu wa njano Usio wakawaida(Abnormal Yellow Discharge)

Kuna hali nyingine ambapo kutokwa na Uchfu ukeni wa njano sio kawaida.  Katika hali kama hizi, mabadiliko ya rangi mara nyingi yatakuwa ya kina zaidi, na kunaweza pia kuwa na hali Zingine zisizo zakawaida kama vile kuwa na harufu mbaya n.k. 

Unaweza kupata dalili zingine ikiwa kutokwa na Uchafu huu ni Ishara ya shida ya kiafya.

Chanzo cha Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni

Haya ni Baadhi ya Magonjwa Pamoja na Hali za kiafya ambazo huweza kusababisha tatizo la Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni;

1. Tatizo la Vaginitis

"Vaginitis" ni neno linalotumiwa kuelezea idadi ya hali ambazo zinaweza kusababisha kuvimba katika uke.  Hali Hizi zinaweza kujumuisha maambukizi yanayotokana na bakteria, virusi, au Fangasi.

Katika baadhi ya matukio, tatizo hili linaweza kusababishwa na athari ya mzio kwa bidhaa kama vile dawa za kupuliza ukeni, douchi, dawa za kuua manii, baadhi ya sabuni n.k

Matumizi ya baadhi ya dawa fulani pia yanaweza kusababisha tatizo la vaginitis. dawa hizi ni pamoja na baadhi ya dawa jamii ya antibiotics na corticosteroids.

Dalili za tatizo hili la Vaginitis ni pamoja na;

  • Kutokwa na UChafu usio wa kawaida Ukeni ambao unaweza kuwa wa rangi ya njano au kijani
  •  Kutokwa na UChafu usio wa kawaida ambao una harufu mbaya
  •  Kupata Maumivu wakati wa kujamiiana
  •  Kuhisi hali ya Kuungua ukeni au wakati wa kukojoa
  •  Kupata Muwasho ukeni
  •  Kutokwa na damu ukeni wakati au baada ya kujamiiana
  •  Kuwasha nje ya uke n.k

2. Tatizo la Trichomoniasis

Trichomoniasis ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na vimelea au parasite.  Ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa yasiyo ya virusi yanayoenea zaidi duniani. 

Ugonjwa huu wa Trikomoniasis hutokana na mtu kupata maambukizi ya vimelea aina ya PROTOZOA vinavyojulikana kwa jina la TRICHOMONAS VAGINALIS

 Unaweza kuwa na trichomoniasis bila kujua kwa sababu maambukizi hayasababishi dalili kila wakati.

 Ila Wakati kuna dalili, trichomoniasis inaweza kusababisha kutokwa na Uchafu ukeni ambayo ni:
  • Mwepesi
  • Kama povu
  • Mweupe,chanjo au kijani
  • Wenye harufu mbaya n.k


3. Magonjwa mengine ya Zinaa ni Chlamydia pamoja na Kisonono

Klamidia na kisonono ni magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na bakteria tofauti.

Magonjwa haya mawili ya zinaa yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu ukeni ambayo ni:
  • Mweupe, njano au kijani
  • Wenye harufu mbaya
  •  Unaweza pia kupata maumivu chini ya tumbo au kitovu 
  • na maumivu au hali ya kuhisi kuungua wakati wa kukojoa.
 Klamidia na kisonono vote hutibiwa kwa dawa jamii ya antibiotics. 


4. Ugonjwa wa PID-Pelvic Inflammatory Disease

Pelvic inflammatory disease (PID) ni maambukizi ya bacteria kwenye via vya Uzazi vya Mwanamke, 
Via hizo vya Uzazi ni pamoja na;Kizazi chenyewe(uterus),mirija ya uzazi yaani fallopian tubes pamoja na vifuko vya mayai au ovaries.

Dalili za Ugonjwa wa PID ni pamoja na;

  • Kutokwa na uchafu ukeni wenye rangi ya kijani,njano n.k
  • Kutokwa na Uchafu ukeni wenye harufu mbaya
  • Kupata Homa
  • Kupata Maumivu ya chini ya tumbo
  • Kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi
  •  Kuhisi hali ya Kuungua wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na damu wakati wa kujamiiana
  • Kupata Maumivu wakati wa tendo n.k

5. Tatizo la kuvimba Mlango wa kizazi-Cervicitis

Cervicitis ni tatizo la kuvimba kwa mlango wa kizazi au Cervix.  Hali hii Inaweza kusababishwa na maambukizi kama vile ya chlamydia, kisonono, pamoja na genital herpes. Hata hivyo, inaweza pia kuwa ni matokeo ya sababu zisizo za kuambukiza kama vile ugonjwa wa ngozi, magonjwa ya kingamwili, na vifaa vinavyowekwa ndani ya uke kama vile IUDs n.k

Mara nyingi tatizo hili halisababishi dalili yoyote wakati wote kwa Nje.  Ila Inapotokea, kunaweza kuwa na kutokwa kwa uchafu unaoendelea, usio wa kawaida ambao ni:
  • Mweupe,Njano au kijani
  • Wenye harufu mbaya n.k

6. Tatizo la Bacterial Vaginosis

Bacterial Vaginosis ni tatizo linalohusisha maambukizi ya bacteria ukeni, na kwa asilimia kubwa hutokana na kuongezeka kwa bakteria wa kawaida kwenye uke(overgrowth) ambao huvuruga usawa wa asili Ukeni au kukosekana kwa uwiano kati ya bacteria wabaya na wale bacteria wazuri waliopo ukeni.

Tatizo hili linaweza kusababisha kutokwa na majimaji ya njano ukeni na dalili zingine zinazohusiana na kutokwa na uchafu usio wa kawaida kama vile:
  • Kutokwa na Uchafu ukeni wenye harufu kali kama shombo la Samaki
  • Kutokwa na Uchafu ukeni wa rangi ya kijani, n.k
Hizo ni baadhi ya Sababu za Kutokwa na Uchafu wa njano ukeni.


Bonus Tips; Nikupe Vidokezo Muhimu juu ya Vitu vya kuzingatia ili kujikinga na Tatizo hili la kutokwa na Uchafu wa njano Ukeni;

- Jikinge na Magonjwa yote ya Zinaa

- Epuka matumizi ya vifaa vya kuingiza ukeni maarufu kama douchi

- Epuka kutumia dawa za kuua Manii

- Hakikisha Usafi mzuri wa Sehemu zako za Siri ikiwa ni pamoja na nguo zako za ndani,kubadilisha PEDI kwa wakati kama upo kwenye hedhi n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!