Chanzo Cha Tatizo La Kuvimba Miguu Na Matibabu Yake

Chanzo Cha Tatizo La Kuvimba Miguu Na Matibabu Yake

Tatizo la kuvimba miguu na vifundo vyake ni shida ya kawaida sana kutokea haswa kwa watu ambao umri umeenda au wazee,

japo siku hizi ni tatizo ambalo huweza kutokea kwa kila mtu. Mkusanyiko usiokuwa wa kawaida wa Majimaji ya mwili au (body fluid) ndani ya Tissues kwenye vifundo na miguu, huweza kusababisha Miguu kuvimba au kwa kitaalam huitwa edema.

Kuwa na shida ya Mkusanyiko wa maji sehemu moja kwenye miguu ambapo tunaita Fluid retention huweza kusababisha hali hii.

Chanzo Cha Tatizo La Kuvimba Miguu

VISABABISHI VYA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU

Zipo Sababu mbali mbali ambazo huleta shida hii,na baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na;

  1.  Kuwa na uzito mkubwa au uliopitiliza huweza kusababisha miguu kuvimba mara kwa mara
  2. Kuambukizwa magonjwa ya miguu ambayo huathiri kusukuma damu vizuri 
  3. Kukaaa kwa Muda Mrefu sehemu Moja Mfano wakati wa Safari Ndefu,watu wengi hupata tatizo la kuvimba miguu
  4. Kusimama kwa muda mrefu, mara nyingi husababisha kuvimba kwa miguu na vifundo vyake
  5. kupata matatizo au magonjwa ya moyo
  6. Kugongwa na kitu,au kuumia kwenye Miguu huweza kusababisha kuvimba
  7. Upasuaji unaojumuisha mguu, au kifundo cha mguu huweza kusababisha kuvimba
  8. Ugonjwa wa Figo, Pia wagonjwa wa Figo huweza kupata shida hii ya kuvimba miguu
  9. Tatizo la Miguu kuvimba linaweza kutokea Pia kwa wanawake WAJAWAZITO au wakati Flani katika mzunguko wa hedhi.  Wanawake wengi  huvimba Miguu wakati wa ujauzito.  Ingawa Uvimbe wa miguu kupita kiasi wakati wa ujauzito inaweza kuwa ishara mojawapo ya Ugonjwa wa kifafa cha Mimba
  10. Miguu  kuvimba inaweza kuwa ishara ya kushindwa kwa moyo kufanya kazi, figo kushindwa kufanya kazi, au ini kushindwa kufanya kazi.
  11. Matumizi ya baadhi ya Dawa;Dawa zingine pia zinaweza kusababisha miguu yako kuvimba:

JINSI YA KUGUNDUA UWEPO WA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU

Wataalam wa afya au Daktari wako atachukua historia ya Tatizo lako,kufanya uchunguzi kamili wa mwili, akizingatia moyo wako, mapafu, tumbo, nodi za limfu,  na miguu kwa ujumla.

Utaulizwa maswali kama haya yafuatayo:

 ➖ Sehemu gani za mwili zinavimba? miguu?  Juu ya goti au chini?

 ➖ Je! Una uvimbe wakati wote au hutokea wakati wa safari,umekaa,umesimama mda mrefu,asubuhi au jioni? 

➖Ni nini ukikifanya uvimbe wako hupungua au kuisha?

 ➖ Ni nini kinachofanya uvimbe wako kuongezeka zaidi?

➖Je! Uvimbe unapungua wakati unainua miguu yako?

 ➖ Je! Una dalili gani zingine?

 Uchunguzi ambao unaweza kufanywa ni pamoja na:

- Vipimo vya damu

 - X-ray ya kifua

- ECG

- Uchunguzi wa mkojo n.k

Vipimo hivo vitakusaidia kujua sababu ya Kuvimba kwa Miguu yako

UKIONA VIASHIRIA KAMA HIVI HAPA CHINI TAFTA MSAADA WA HARAKA

Hali ya Kuvimba Miguu inaambatana na Dalili hizi;

(1) Unajisikia kukosa pumzi.

 (2) Unapata maumivu ya kifua, kifua kuwa kizito au kubana.

 (3) Una ugonjwa wa moyo au ugonjwa wa figo na Kuvimba kunazidi kuongezeka

 (4) Una historia ya ugonjwa wa ini na sasa unapata tatizo la kuvimba miguu yako au tumbo.

(5) Mguu wako umevimba na unabadilika rangi na kuwa mwekundu au unahisi hali ya kuwaka moto sana hasa ukiushika.

 (6) Unavimba Miguu na Unapata homa.

 (7) Wewe ni mjamzito na miguu umevimba kupita kiasi.

MATIBABU YA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU

-Inua miguu yako juu wakati umelala chini. Zoezi hili husaidia kusukuma maji kutoka kwenye miguu yako kurudi sehemu ya juu ya mwili wako,hivo kuondoa Uvimbe miguuni,Ingawa hii inaweza isiwe tiba ya kudumu kulingana na chanzo husika.

 - Wakati wa kusafiri,mara nyingi jitahidi uwe unasimama na kuzunguka mara kwa mara, Ikiwa shida ya kuvimba Miguu hutokea wakati wa Safari.

- Epuka kuvaa mavazi ya kubana sana Miguu au eneo karibu na mapaja yako.

 - Punguza uzito wa mwili ikiwa inahitajika

 - Epuka matumizi ya dawa zozote ambazo zinaweza kusababisha tatizo la kuvimba Miguu

- Pia Tiba zingine kama Dawa,Upasuaji n.k, kulingana na sababu au chanzo cha Tatizo hili la miguu kuvimba huweza kuhitajika 

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!