Faida ya supu ya kuku,Soma hapa kila kitu
Je,unapenda Supu ya Kuku? Umewahi kusikia kama wengine huitumia kama dawa? Je,Supu hii ya kuku ina Siri gani ndani yake? Leo katika afyaclass,tumechambua baadhi ya Faida za Supu ya Kuku Mwilini.
Faida ya supu ya kuku
Supu ya kuku imekuwa suluhisho la watu wengi pale ambapo huitumia kama Dawa ya Mafua kwa karne nyingi, Hata hivyo, je, kuna sayansi yoyote inayounga mkono sifa yake kama tiba ya kumsaidia Mtu kujisikia vizuri? Jibu linaweza kukushangaza.
Makala hii inachambua kwa kina zaidi kuliko tu kuitumia kama chakula au mchuzi wa nyama ya kuku, Makala hii inaangazia manufaa mbalimbali ya kiafya ya supu ya kuku.
Hizi hapa ni Faida Mbali mbali za Supu ya Kuku;
1. Supu ya kuku husaidia Kuongeza Maji mwilini
Kuwa na maji ya kutosha mwilini ni muhimu kwa afya ya mwili kwa ujumla, Supu ya kuku, pamoja na faida yake kama mchuzi, ni njia ya ajabu ya kusaidia kuongeza maji mwilini, hasa wakati wa kupambana na baridi au mafua.
Kioevu hicho chenye joto hutuliza maumivu ya koo na husaidia kupunguza msongamano kooni,hii pia hukusaidia kukabiliana na upungufu wa maji mwilini endapo utahisha njia za kula vitu vingine vya kuongeza maji mwilini.
2. Supu ya kuku ina Electrolytes za kutosha
Electrolytes ninazozungumzia hapa ni madini kama sodiamu na potasiamu ambayo ni muhimu katika kazi mbalimbali za mwili, ikiwa ni pamoja na kuimarisha misuli na nerves.
Wakati unaumwa, unaweza kupoteza elektroliti kupitia jasho,ukiwa na homa n.k. Supu ya kuku inaweza kusaidia kujaza elektroliti hizi zilizopotea, na kuimarisha afya kwa Ujumla.
3. Supu ya kuku huweza kupambana na vimbe mbali mbali(Anti-Inflammatory Powerhouse)
Supu ya kuku ina viambato kama anti-inflammatory compounds vya asili ambavyo huweza kusaidia kupunguza kuvimba, kuwa Msaada kwa Mtu mwenye ugonjwa wa arthritis na masuala ya kupumua.
4. Supu ya Kuku huweza kuimarisha kinga ya Mwili(Immune System Support)
Supu ya Kuku ina protini, muhimu kwa ajili ya kujenga na kurekebisha tishu, wakati mboga kama karoti na vitunguu hutoa vitamini na antioxidants ambavyo vyote kwa Ujumla husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwili.
5. Supu ya kuku ni Msaada kwa Watu wenye mafua au Pua Kuziba
Mvuke wa joto kutoka kwenye supu ya kuku unaweza kusaidia kushusha kamasi na kuondoa msongamano au hali ya kuziba katika vitundu vya pua. Hii inaweza kusaidia hasa wakati wa kupambana na tatizo la Mafua.
6. Supu ya kuku Msaada kwa Watu wenye maumivu ya koo,hali ya vidonda kooni(Sore Throat) n.k
Mchuzi wa moto wa supu ya kuku unaweza kupunguza maumivu ya koo na kupunguza usumbufu. Kutumia kioevu hiki chenye joto kunaweza pia kusaidia kupunguza maumivu na hali ya kuwasha kooni.
7. Supu ya kuku ni rahisi kumeng'enywa
Supu ya kuku ni chakula rahisi sana kumeng'enywa mwilini, Hii ni muhimu hasa wakati mwili wako unapambana na ugonjwa ambao hauwezi kuvumilia vyakula vizito.
8. Supu ya kuku ni Chanzo cha Virutubisho vingi mwilini(Source of Essential Nutrients)
Vipo virutubisho vingi ambavyo tunaweza kuvipata kwenye Supu ya Kuku, Virutubisho hivo ni pamoja na;
- Protein,
- Vitamins,
- Madini kama Potassium, Sodium n.k
Hizi ni Faida Chache ambazo tumechambua katika Makala hii..... Asante....!!!!!
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!