Mama mjamzito kuchoma sindano ya Anti D

Mama mjamzito kuchoma sindano ya Anti D


UCHOMAJI WA SINDANO YA ANTI-D(Rho) KWA MAMA MJAMZITO NA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA

 Baada ya mama mjamzito kuanza Kliniki na kupima group la Damu,moja ya vitu vikubwa ambavyo wataalam wa afya huangalia ni pamoja na Rhesus factor ya mama na baba,ambapo huweza kuwa POSITIVE au NEGATIVE,mfano kwenye makundi ya damu utaona yameandikwa hivi; A+ au A-, B+ au B-, AB+ au AB-, O+ au O-, hizo positive na negative ndyo tunasema Rhesus factors.

Sasa basi, endapo Baba ana kundi lolote la damu Rhesus factor positive mfano; A+,B+,AB+ au O+, na mama mjamzito akawa na kundi lolote la damu rhesus factor negative mfano; A-,B-,AB- au O-, hapa tayari kuna tatizo,

Mama huyu mjamzito yupo kwenye hatari ya kupatwa na matatizo kama vile; mimba kutoka zenyewe au kuzaa mtoto mwenye matatizo kama vile kukosa hewa ya oxygen kwenye ubongo,mtoto kuishiwa na damu,mtoto kufariki muda mfupi baada ya kuzaliwa pamoja na matatizo mengine yanayohusu damu yaani hemolytic diseases hasa kwenye ujauzito wake wa pili.

Sasa kutokana na matatizo hayo,ndipo swala la kutumia sindano za Anti-D linapoanza ili kumsaidia mama huyu pamoja na ujauzito wake aliyobeba kumkinga na matatizo hayo.

UCHOMAJI WA SINDANO YA ANTI-D(Rho) KWA MAMA MJAMZITO NA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA

Anti-D(Rho) Immunoglobulin(monoclonal) injection, sindano hii huchomwa kwa mama ili kumsaidia asipatwe na matatizo ambayo tayari nimekwisha kueleza hapo juu,

Sindano ya Anti-D ni sindano ambayo hutoa Anti-D immunoglobulin kwenye damu ya mama Mjamzito na mama baada ya kujifungua,

Kazi kubwa ya anti-D immunoglobulin ni kusaidia kuneutralises Antigens zozote zinazotokana na Rhesus factor(RhD) positive,

Antigens hizi huingia kwenye mzunguko wa damu wa mama wakati wa Ujauzito,

Endapo antigens hizi zimefanikiwa kuzimwa au kufanyiwa neutralization,haziwezi tena kusababisha damu ya Mama kutengeneza antibodies kwa ajili ya mapambano.

DOSE ZA SINDANO YA ANTI-D(Rho) KWA MAMA MWENYE BLOOD GROUP AMBAZO ZINA MATATIZO NILIYOELEZEA HAPO JUU

1. Dose ya kwanza ya sindano za Anti-D, huchomwa kwa mama mjamzito ambaye ujauzito wake una umri wa kuanzia MIEZI SABA(7) au Wiki 28-30 za ujauzito,

Hivo basi, mama mjamzito atachomwa sindano yenye 1500 IU~300mcg IV/IM,ujauzito ukiwa na miezi saba au kuanzia wiki 28-30 za ujauzito

2. Dose ya pili ya Sindano ya Anti-D huchomwa ndani ya Masaa 72 baada ya mama kujifungua,

Hivo basi, mama Baada ya kujifungua atachomwa sindano yenye 1500 IU~300mcg IV/IM,ndani ya MASAA 72 baada ya kujifungua,

Lakini wataalam wa afya hushauri kwamba,endapo mama hakufanikiwa kuchoma sindano ya ANTI-D ndani ya masaa 72 baada ya kujifungua anatakiwa ahakikishe kachoma hyo sindano Ndani ya siku 28,ila asiache kabsa kuchoma.

KUMBUKA; mama kuchoma dose zote mbili yaani wakati wa ujauzito na ndani ya masaa 72 baada ya kujifungua hutoa matokeo mazuri zaidi kuliko kwa mama ambaye kachoma dose moja tu ya Anti-D.

Lakini pia kama seli nyekundu za damu kwa mtoto aliyetumboni kwa mama yake( FETAL RED BLOOD CELLS(RBC), zina >15ml Rho+, doses zaidi ya mbili za anti-D 1500 IU huweza kutumika,ila hii ni special cases.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!