Sababu Za Uke Kuwa Mkavu Na Tiba Yake

Sababu Za Uke Kuwa Mkavu Na Tiba Yake

Tatizo hili la mwanamke kuwa na uke mkavu linawapata wanawake wengi sana kwa hivi sasa, ambapo wengine hupata madhara mbali mbali kama maumivu makali wakati wa tendo la Ndoa N.K.

Tatizo hili huweza kuhusishwa na sababu mbali mbali ikiwemo ile ya baadhi ya magonjwa,mabadiliko ya vichocheo mwilini N.K. Sababu za mwanamke kuwa na uke mkavu zimeelezewa vizuri hapa chini;

Chanzo cha Uke kuwa Mkavu

SABABU ZA MWANAMKE KUWA NA UKE MKAVU NI PAMOJA NA;

1. Mvurugiko wa vichocheo mwilini yaani kwa kitaalam Hormone imbalance, hasa hasa vichocheo aina ya ESTROGEN ambavyo huhusika kwa kiasi kikubwa kuleta hali ya unyevu unyevu,ute pamoja na ulainishi ndani ya sehemu za siri za mwanamke.

2. Matumizi ya baadhi ya vitu vyenye kemikali katika kusafisha sehemu za siri za mwanamke Mfano; baadhi ya Sabuni.n.k

3. Kupatwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali ya zinaa Kama vile; Ugonjwa wa kisonono au kaswende.

4. Kupatwa na maambukizi katika njia au mfumo Mzima wa mkojo wa mwanamke yaani Urinary track infection(UTI).

5. Kuwa na tatizo la Fangasi ambazo haziishi,zinazojirudia rudia mara kwa mara licha ya matumizi ya dawa nyingi.

6. Mwanamke kupatwa na maambukizi ya bacteria katika via vyake vya uzazi yaani PELVIC INFLAMMATORY DISEASE(PID) n.k

Dalili za Uke kuwa Mkavu

DALILI ZA TATIZO LA MWANAMKE KUWA NA  UKE MKAVU NI PAMOJA NA;

• Kupatwa na maumivu makali Ukeni wakati wa kufanya mapenzi

• Kupatwa na maumivu ya kiuno baada ya kufanya mapenzi

• Kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa,hiki ni kiashiria cha uke mkavu,pamoja na kutokea kwa michubuko wakati wa tendo la ndoa.

• Mwanamke kupoteza hamu ya kufanya mapenzi

• Kuwa na hali ya kukamaa pamoja na ukavu katika sehemu za siri za mwanamke n.k

Madhara ya Uke kuwa Mkavu

MADHARA YA MWANAMKE KUWA NA TATIZO LA UKE MKAVU NI PAMOJA NA;

✓ Mwanamke Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

✓ Mwanamke kukosa hamu kabsa ya tendo la ndoa

✓ Kupata michubuko wakati wa tendo la ndoa

✓ Kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa ukimwi pamoja na magonjwa mengine ya zinaa kutokana na hali ya michubuko ukeni

✓ Mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maambukizi katika via vyake vya uzazi yaani PID

✓ kutokwa na damu ukeni wakati wa kufanya mapenzi

MATIBABU YA TATIZO LA MWANAMKE KUWA NA UKE MKAVU

- Matibabu ya tatizo la uke mkavu hutegemea na chanzo cha tatizo husika hivo basi ni vizuri kuongea na wataalam wa afya ili kuweza kujua chanzo cha uke mkavu pamoja na matibabu yake.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!