Tatizo la miguu kuwaka moto,chanzo na Tiba
Tatizo la Miguu kuwaka moto au kuwa na Hisia za kuungua(burning sensation) kwenye ngozi, misuli, au mishipa ya damu miguuni inaweza kutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo uharibifu wa nerves, na mambo mengine. Soma makala hii mpaka mwisho tumeeleza kila kitu.
Tatizo la Miguu kuwaka moto huweza kuambatana na hisia ya joto kali au kuungua, kutetemeka, kuchoma choma au Miguu kufa ganzi. Hisia hizi zinaweza kuwa katika mguu mmoja, miguu yote, au sehemu ya mguu tu,
Mgonjwa Kuelezea maumivu na eneo husika hali ya kuungua inapotokea kunaweza kusaidia daktari kufanya uchunguzi Sahihi Zaidi.
Makala hii inazungumzia sababu zinazoweza kusababisha tatizo hili, dalili za ziada, na wakati wa kumuona daktari.
CHANZO CHA MIGUU KUWAKA MOTO NI NINI?
Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo la miguu kuwaka moto kama vile;
- Mtu kuwa na ukosefu wa kutosha wa vitamins mwilini kama vile; Vitamin B n.k
- Kuwa na tatizo la upungufu wa vichocheo vya thyroid shingoni
- Kuwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali yanayoshusha kinga ya mwili kama Ukimwi n.k
- Kuwa na tatizo la Ugonjwa wa Kisukari
- Mtu Kuwa na matitizo ya Figo
- Mtu kuwa na tatizo la Fangasi wa miguuni
- Kuharibika kwa mfumo wa Nerves maeneo ya miguuni
- Kuwa na tatizo la Saratani pamoja na matumizi ya baadhi ya dawa za kutibu tatizo hili n.k
Sababu Zingine ni Pamoja na;
• Kufanya Mazoezi
Mazoezi ambayo hutumia misuli ya kwenye miguu yanaweza kusababisha hali hii ya Miguu kuwaka Moto. Hii haimaanishi kila wakati kuwa misuli imejeruhiwa.
Wakati wa mazoezi haya yanayohusisha sana miguu, mwili unahitaji nishati zaidi kuliko kawaida. Hapa mwili hauwezi kuchukua oksijeni ya kutosha kuunda nishati, kwa hivyo misuli ya mwili inachukua nafasi. Hii inasababisha kutengenezwa kwa lactic acid, ambayo husababisha hisia ya kuwaka moto kwenye miguu.
Hata hivo hali hii mara nyingi sio tatizo kubwa na huisha yenyewe ndani ya muda mfupi,ikiwa imekuwa tatizo endelevu hakikisha unapata Msaada kwa Wataalam wa afya, au kwa Ushauri Zaidi,elimu na Tiba tuwasiliane hapa hapa ndani ya afyaclass kupitia namba +255758286584.
• Kuumia au kupata majeraha,Injury
Kuumiza mguu ni moja ya sababu za kawaida za kupata maumivu, na ikiwa uharibifu wa misuli umetokea unaweza kusababisha Tatizo la Miguu kuwaka moto.
• Tatizo la Uharibifu wa mishipa ya Fahamu au Nerve damage
Uharibifu wa Nerves kwenye maeneo kama vile Miguuni ambapo kwa kitaalam tunaita Peripheral neuropathy huweza kusababisha tatizo la Miguu kuwaka Moto,
Na moja ya magonjwa ambayo husababisha hali hii kwa kiasi kikubwa ni pamoja na Ugonjwa wa Kisukari ambapo husababisha hali ambayo tunaita Diabetic neuropathy.
Sukari kuwa kwa kiwango kikubwa kwenye damu kutokana na ugonjwa wa kisukari huharibu neva na mishipa ya damu inayolisha nerves husika.
• Sababu Zingine za Tatizo la Miguu kuwaka moto ni pamoja na;
- Kuwa na Uvimbe
- Mgandamizo mkubwa au Presha kwenye mishipa ya Miguu n.k
NB:Hakikisha Unakutakana na Wataalam wa afya Mara Moja ikiwa Tatizo la Miguu kuwaka Moto Linaambatana na Dalili hizi;
- Miguu kuwa na Malengelenge au Vidonda
- Unapata homa,maumivu makali ya Kichwa
- Unapata dalili za kama kuchanganyikiwa
- Unahisi kichefuchefu na kutapika
- Hali ya Miguu kuwaka Moto inazidi kuongezeka siku hadi siku n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!