Ugonjwa Usiojulikana waua watu 27 Congo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza jana December 05,2024 kuwa iko katika tahadhari ya juu kutokana na kuzuka kwa ugonjwa usiojulikana ambao umesababisha vifo vya Watu kadhaa ndani ya muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Mtandao wa DW Kiswahili umeripoti kuwa Waziri wa Afya wa Nchi hiyo, Samuel Roger Kamba amewaambia Waandishi wa Habari Mjini Kinshasa kuwa Mamlaka iko macho na kwamba wanafuatilia mlipuko wa ugonjwa huo kwa ukaribu sana.
Waziri huyo amesema jana kuwa wamehesabu miili ya Watu 27 katika vituo vya afya waliofariki kutokana na ugonjwa huo ambao unasababisha dalili zinazofanana na mafua makali ambazo ni homa, kikohozi na maumivu ya kichwa.
Ugonjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi October mwaka huu na hadi sasa umeripotiwa zaidi katika eneo la Panzi, takriban kilomita 700 kusini mashariki mwa mji mkuu Kinshasa.
Kamba amesema Watu wengine 44 wameripotiwa kufariki pia lakini ameweka bayana kuwa huenda vifo hivyo vimetokana na sababu nyingine.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!