Ukimwi huambukizwa kwa njia gani
Unaweza kupata Virusi vya Ukimwi(VVU) tu kwa kugusana moja kwa moja na viowevu fulani vya mwili(body fluids) kutoka kwa mtu aliye na VVU, Viowevu hivo ni pamoja na:
- Damu
- Shahawa na majimaji kabla ya shahawa
- Majimaji kutoka kwenye rectum
- Majimaji ya ukeni
- Maziwa ya mama n.k.
Kumbuka hili; Ili Maambukizi kutokea, VVU katika viowevu hivi(Body fluids) lazima viingie kwenye mkondo wa damu wa mtu asiye na VVU,
Kwahyo Virusi huweza kupenya kutoka kwenye vyanzo hivi kupitia utando wa mucous (unaopatikana kwenye puru, uke, mdomo, au ncha ya uume), kupitia mikato,majeraha yoyote au vidonda au Ukiwa na michubuko, au kupitia sehemu ulizochomwa na vitu vyenye ncha kali kama vile sindano,kukatwa na nyembe n.k.
Ukimwi huambukizwa kwa njia gani
Hizi hapa ni njia kubwa ambapo Ukimwi huweza kuambukizwa kutoka kwa Mtu mmoja kwenda kwa mwingine;
1. Kwa kufanya ngono Zembe, kufanya mapenzi bila kinga kama Condomu na Mtu ambaye tayari ana maambukizi.
2. Kufanya Mapenzi kinyume na maumbile(Anal sex),
Watu wanaofanya hivi wapo kwenye hatari kubwa Zaidi ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
3. Kushare Vifaa vya ncha kali kama vile nyembe,Sindano n.k. Kupata majeraha,vidonda au kuumia kwa namna yoyote hasa maeneo kama mdomoni,sehemu za siri au eneo la haja kubwa huweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi ikiwa utashiriki tendo na mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
4. Kutoka kwa Mama mjamzito kwenda kwa Mtoto,
Mama aliye na VVU anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito, kuzaliwa, au kunyonyesha. Hata hivyo, matumizi ya dawa za VVU na mikakati mingine imesaidia kupunguza hatari ya maambukizi ya VVU wakati wa kujifungua au kutoka kwa mama kwenda kwa Mtoto wakati wa kunyonyesha.
5. Wakati wa Uchangiaji Damu(blood transfusions),
Unaweza kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiwa umepewa damu au kuchangiwa damu ya Mtu ambaye tayari kaathirika na virusi vya Ukimwi(VVU).
6. lakini pia zipo baadhi ya Cases ambapo watu hupata maambukizi kwa Njia kama vile;
- Kushare Miswaki
- Kugh'atwa na Mtu mwenye maambukizi n.k
Hizo ni baadhi ya Njia Chache ambazo Watu huweza kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU).
Rejea Link|Source: https://www.hiv.gov/hiv-basics/overview/about-hiv-and-aids/how-is-hiv-transmitted
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!