Vidonge sio njia nzuri ya kuzuia mimba kwa Muda mrefu
Hata Kama Vinazuia Mimba,Vidonge sio njia nzuri ya kuzuia mimba kwa Muda mrefu.
Mfano;Ikiwa unataka kuzuia mimba kwa muda wa miaka 2 au 3, kama unatumia vidonge vya uzazi wa mpango,itakulazimu umeze kila siku kidonge1 kwa Muda wa miaka 3.
Kumbuka,tafiti mbali mbali zinaonyesha matumizi ya Muda Mrefu sana na njia hii huweza kuongeza hatari ya Mtu kupata Saratani ikiwemo Saratani ya Mlango wa kizazi(Cervical cancer).
Unashauriwa hata kama Unatumia vidonge vya Uzazi wa Mpango basi isiwe ndyo njia yako ya Muda mrefu kwa ajili ya kupanga Uzazi,
Usitumie njia hii ya vidonge kwa muda mrefu zaidi Mfano kwa Miaka 3, Miaka 5 n.k
Kadiri mwanamke anavyotumia vidonge vya kupanga Uzazi(Oral contraceptive piils) kwa muda mrefu, ndivyo hatari ya kupata saratani ya Mlango wa kizazi inavyoongezeka.
Utafiti mmoja uligundua hatari ya Mwanamke kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi(Cervical Cancer) iliyoongezeka kwa asilimia 10% kwa wanawake waliotumia Vidonge kwa muda wa chini ya miaka 5,
Lakini hatari iliyoongezeka zaidi kwa asilimia 60% kwa wanawake waliotumia Vidonge kwa Muda wa miaka 5 mpaka 9,
na kuongezeka maradufu kwa hatari dhidi ya wanawake waliotumia Vidonge vya Uzazi kwa Muda wa miaka 10 au zaidi.
Mwanamke aliyetumia Vidonge vya Kupanga Uzazi kwa Muda wa Miaka 5 au Zaidi,yupo kwenye hatari zaidi ya Kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi(Cervical cancer) kuliko Mwanamke ambaye hajawahi kabsa kutumia Vidonge.
Ingawa pia,hatari ya saratani ya Mlango wa kizazi imeonekana kupungua baada ya muda kwa wanawake ambao waliacha kutumia vidonge vya Uzazi wa mpango kwa muda wa miaka 10 mpaka 12.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!