Mjamzito Anaweza Kufanya Tendo La Ndoa

Mjamzito Anaweza Kufanya Tendo La Ndoa

JE KUNA MADHARA YOYOTE ENDAPO MAMA MJAMZITO AKIFANYA TENDO LA NDOA?

Hakuna madhara yoyote endapo mama mjamzito atafanya tendo la ndoa ikiwa mama huyo hana tatizo lolote, Hivo katika kufanya tendo la ndoa kwa mjamzito kuna angalizo, inaweza kuwa Salama au isiwe Salama kulingana na hali ya mama mjamzito husika.

tuangalie matatizo ambayo huweza kupelekea iwe vigumu kwa mama mjamzito kufanya tendo la Ndoa.

Matatizo ambayo huweza kusababisha Mama mjamzito asifanye Tendo la Ndoa(Pregnancy complications)

Ikiwa una matatizo ya ujauzito, kama vile kupata leba kabla ya wakati(preterm labor) au matatizo kwenye kondo la nyuma(placenta), unapaswa kuzungumza na daktari wako akuangalie na kutoa majibu ikiwa ni salama kwako kufanya tendo la ndoa ukiwa mjamzito au la. 

Yapo baadhi ya matatizo ambayo huweza kuweka zuio la wewe kushiriki tendo la ndoa ukiwa mjamzito, na matatizo hayo ni kama vile;

1. Kuvuja damu sana

Unapaswa kuepuka kufanya tendo la ndoa ukiwa mjamzito ikiwa una tatizo la kutokwa na damu nyingi, kwani  kufanya hivo inaweza kuongeza hatari ya kutokwa na damu zaidi,

Lakini pia sio salama kushiriki tendo la ndoa ukiwa mjamzito ikiwa una tatizo la damu kushindwa kuganda yaani coagulopathy n.k,

2. Chupa ya Uzazi kupasuka

Ikiwa wewe ni mjamzito na chupa ya Uzazi imepasuka, Unapaswa kuepuka kufanya tendo la ndoa, kwani inaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi(infections). 

3. Kuwa na matatizo kwenye shingo ya kizazi(Cervical problems)

Mjamzito Unapaswa kuepuka kufanya tendo la ndoa ikiwa una matatizo yoyote kwenye shingo ya kizazi chako, kwani unaweza kuwa katika hatari kubwa ya kupata leba mapema,

Matatizo hayo ni pamoja na Shingo ya kizazi kulegea na kushindwa kuhimili ujauzito n.k.

4. Kupata Leba mapema au kabla ya wakati, Mimba kuharibika zenyewe n.k

Kwa mama mjamzito mwenye matitizo kama haya ni vizuri kuongea na Wataalam wa afya na kupewa Ushauri sahihi wa jinsi ya kushiriki tendo la ndoa.

HIVO; kufanya tendo la ndoa endapo huna tatizo lolote lile wakati wa ujauzito ni salama kabsa kwako

Bonus Tips; MAMA MJAMZITO AZINGATIE HAYA;

- Mahudhurio ya Kliniki kwa mama mjamzito ni muhimu sana

-  Mjamzito Apende kulala ubavu, hasa ubavu wake wa kushoto kuliko kulalia mgongo, na hili lifanyike hasa ujauzito ukiwa mkubwa

- Mjamzito Asivae nguo za kumbana sana, viatu virefu,mikanda tumboni n.k

- Mjamzito Apende kufanya mazoezi mara kwa mara, ujauzito sio ugonjwa,kiasi kwamba muda wote unalala kitandani.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!