Kusambaratika kwa programu za kuzuia na kukabiliana na HIV
Uamuzi wa Serikali ya Trump kusitisha misaada ya kigeni iliyokuwa ikisimamiwa na Shirika la misaada la Marekani USAID imeathiri usambazaji na matibabu ya virusi vya VVU kwa nchi nyingi, ambazo kutakuwa na uhaba wa dawa za kupunguza makali ya virusi hivi, Shirika la Afya duniani WHO laonya.
Kusambaratika kwa programu za kuzuia na kukabiliana na HIV huenda kukalemaza juhudi zilizoafikiwa ndani ya miaka 20 ,'' Mkurugenzi Mtendaji wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema hayo katika kikao na wanahabari.
Alisema kuwa Shirika hilo lina wasiwasi kwani upungufu wa dawa hizi za VVU utasababisha maambukizi mapya milioni 10 na vifo milioni tatu vilivyochochewa na makali ya VVU.
Juhudi za kukabiliana na magonjwa kama vile VVU, Malaria, Kifua kikuu na Polio zimeathirika pakubwa baada ya Trump kusitisha misaada ya kigeni iliyoelekezwa kwa programu hizo dakika chache baada ya kuingia katika ikulu ya White House.Via Bbc
KARIBU DISCUSSION CORNER,WEKA MTAZAMO WAKO HAPA KWENYE COMMENT SECTION,JUU YA HILI
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code