Meno ya Mtoto kuwa na nafasi au kuachana

Meno ya Mtoto kuwa na nafasi au kuachana

#1

Meno ya Mtoto kuwa na nafasi au kuachana



Hali ya Meno ya Mtoto mchanga kuachana au kuwa na Nafasi wakati yanaota ni hali ambayo kitaalam hujulikana kama diastema,

Hivo basi,diastema ni pengo au nafasi kati ya meno yoyote mawili, lakini hali hii ni kawaida zaidi au hutokea Zaidi kati ya meno ya juu ya mbele.

Chanzo cha Meno ya Mtoto kuwa na Nafasi

Sababu ya kawaida kwa meno ya mbele kuwa na nafasi wakati yanaota ni fraenum ambayo hukaa chini kuliko kawaida na kutenganisha meno mawili ya juu.  Fraenum ndani ya mdomo wa juu ni mkunjo wa ngozi unaoshikanisha mdomo wa juu na ufizi wa juu.  Ikiwa unainua mdomo wako wa juu, unapaswa kuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa urahisi. 

Fraenum; ni kipande cha tishu nyembamba, kama kamba ambacho huunganisha sehemu mbili za mwili, kama vile Sehemu ya Lips za mdomo na ufizi, au ulimi na sakafu ya mdomo.

Sababu Zingine za Meno kuwa na Nafasi wakati wa Ukuaji wa Mtoto ni pamoja na;

1. Hali ya kawaida ya Uotaji wa Meno(natural teeth development) – Meno ya watoto mara nyingi huwa na Nafasi kati yao ili kutoa nafasi kwa meno makubwa kupitia, hapa nazungumzia meno ya awamu ya pili(adult teeth).

Meno kwa kawaida huwa na nafasi kati yao yanapotokea kwa mara ya kwanza, lakini kuwasili kwa meno ya watu wazima zaidi au Adult teeth hasa meno aina ya canine teeth,  Mara nyingi husaidia kuziba mapengo yoyote.

Hivo Ni kawaida kwa mtoto mdogo kuwa na meno yaliyoachana au kuacha nafasi. Hii hutokea kwa sababu meno ya kwanza (meno ya maziwa-Milk teeth) ni madogo na hutokea katika nafasi ndogo, wakati fizi za mtoto bado zinaendelea kukua. Nafasi hizi husaidia meno ya kudumu (meno ya pili-Adult teeth) kupata nafasi ya kuota vizuri kadri mtoto anavyokua. Kadri mtoto anavyokomaa na meno ya kudumu yanavyotokea, mara nyingi nafasi hizi hupungua au kutoweka kabisa.



2. Kutokuwepo kwa baadhi ya Meno(missing teeth)– Watoto wengine huzaliwa wakiwa wamekosa jino moja au mawili (milk tooth au Adult tooth) kwenye taya zao, jambo ambalo huacha nafasi.  Wakati mwingine meno haya yamekwama kwenye mfupa na hayatoki kupitia nafasi iliyoachwa,

Hii huweza kusababisha kuwepo kwa Nafasi kubwa Zaidi kwenye Meno ya Mtoto.

3. Kuwa na Meno Madogo Sana(small teeth) – Baadhi ya watoto wengine au hata watu wazima wanaweza kuwa na meno madogo sana ambayo huruhusu uwepo wa nafasi kati ya Jino na Jino.

4. Sababu Zingine ni pamoja na;

  • Mfupa wa Taya kuwa mkubwa(large jaws) – baadhi ya taya ni kubwa ikilinganishwa na ukubwa wa meno, hali ambayo hupelekea kuonekana kwa nafasi
  • Kutokuwa na mpangilio mzuri kati ya Meno na taya; meno na taya hazishikani vizuri ambapo kuna tofauti kati ya ukubwa au umbo la taya na mpangilio wa meno.

5. Pia kwa baadhi ya Watoto wenye tatizo la tongue-tie, ile tishu ya fraenum huweza kusababisha pengo au nafasi katika meno ya mbele ya taya ya chini.

KUMBUKA; Nafasi au Mapengo katika meno yanaweza kuziba yenyewe

Mapengo kati ya meno ya mtoto ni ya kawaida sana.  Katika hali nyingi, mapungufu haya yanaweza kujifunga yenyewe kwa kadri ya ukuaji wa Mtoto.

 Wakati meno ya mtoto yanapoanza kutoka (takriban miezi sita hadi tisa), meno ya mbele yanaweza kuwa na mwanya na tishu ya fraenum inaweza kushikamana chini kwenye ufizi.  Mtoto anapofikisha mwaka mmoja, fraenum inaweza kuwa imefupishwa, na meno zaidi yanaweza kuwa yamepita na kuziba mianya yoyote.

Hivo,Mapengo kati ya meno, mara nyingi hujifunga yenyewe kadiri meno ya watu wazima zaidi au Adult teeth yanavyoota. 

Approved Sources|Rejea Links:

https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/conditionsandtreatments/teeth-gapped-teeth

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code