Mitindo ya nywele na hatari ya kupata saratani,Utafiti mpya wabaini

Mitindo ya nywele na hatari ya kupata saratani,Utafiti mpya wabaini

#1

Mitindo ya nywele na hatari ya kupata saratani,Utafiti mpya wabaini



Mitindo ya nywele ya kusuka kwa kuongezea nywele zingine bandia ama asili ni maarufu sana kwa wanawake weusi, ikiendelea kupendwa na watu mashuhuri na akina mama wengi. Lakini sasa, maswali yanaibuka kuhusu athari zake kwa afya yetu.

Mchakato wa kusuka unaweza kuchukua hadi saa tano, ambapo watalamu wa nywele hugawanya sehemu ndogo za nywele kwa ustadi na kuziunganisha na nyongeza za nywele bandia.

Licha ya muda mrefu unaohitajika saluni, ususi umekuwa ukihusiana na urahisi kwa upande wangu.

Nilipokuwa mdogo, ususi ulikuwa kwa ajili ya likizo, kwani mtindo huu uliniwezesha kuogelea bila kuhofia nywele zangu kuvurugika.

Hadi sasa, mimi bado nachagua ususi ninapotaka kupumzika kwa miezi michache bila kusumbuka na kufumua nywele, au ninapotaka kujaribu rangi mpya bila kuhatarisha afya ya nywele zangu kwa kutumia rangi ya kudumu.

Hata hivyo, utafiti mpya unaonyesha kuwa nywele bandia zinazotumiwa na wanawake wengi weusi zinaweza kuwa na madhara kwa afya zao.

Shirika lisilo la faida la Marekani, Consumer Reports, lilifanya majaribio kwa sampuli kutoka kwa aina 10 kumi maarufu za nywele bandia za kusuka na kugundua kuwa zote zilikuwa na kemikali zinazoweza kusababisha saratani, na nyingine zilikuwa na madini ya risasi.

Mara baada ya ripoti hiyo kuchapishwa, mitandao yangu ya kijamii na makundi ya WhatsApp yalijaa 'linki' za ripoti hiyo, zikionya kuhusu hatari zilizofichwa kwenye nywele zetu.

James Rogers, mkuu wa majaribio ya usalama wa bidhaa katika Kampuni ya Consumer Reports, alisema matokeo haya ni ya kutia hofu kwa sababu wanawake wanakuwa katika mgusano wa moja kwa moja na kemikali hizi hatari kwa muda mrefu wanapokuwa na nywele zao zilizofumwa na kusukwa vichwani mwao.

"Tunaamini kwamba kila unapokutana na kemikali hatari, madhara yake hujilimbikiza na huongezeka baada ya muda."

Hata hivyo, alisisitiza kuwa utafiti zaidi unahitajika, akisema: "Tunatumai hii itaanzisha mjadala, siyo tu katika ngazi ya udhibiti, bali pia ndani ya jamii zetu, kuhusu umuhimu wa kupata taarifa sahihi."

Via:Bbc

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code