Mwanaume wa kwanza duniani kupandikiziwa chipu kwenye ubongo Afunguka haya!
Mwanaume wa kwanza duniani kupandikiziwa chipu ya kusoma mawazo kwenye ubongo wake kupitia kampuni ya Elon Musk ya Neuralink ameanza kushuhudia matokeo ya teknolojia hiyo ya kisasa ambapo teknolojia hii inadaiwa kuwa hatua kubwa katika utafiti wa muingiliano kati ya Ubongo wa Binadamu na kompyuta ikilenga kusaidia Watu wenye ulemavu wa mwili kuwasiliana na mazingira yao kwa urahisi zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Neuralink chipu hiyo imewekwa kwa mafanikio na tayari inatoa ishara kuwa inaweza kuchukua mawazo ya Mtumiaji na kuyatafsiri katika mfumo wa kidijitali, Mwanaume huyo ambaye jina lake halijatajwa ameripotiwa kuwa anaweza kutumia akili yake kuendesha mifumo ya kompyuta bila kugusa kifaa chochote, jambo linaloonekana kama mapinduzi makubwa katika sayansi ya neva na uhandisi wa matibabu.
Elon Musk ambaye ndiye mwanzilishi wa Neuralink ameeleza kuwa chipu hii inalenga kusaidia Wagonjwa walio na matatizo ya mfumo wa neva kama vile wale waliopooza kutokana na ajali au maradhi pia Musk amedokeza kuwa teknolojia hii inaweza kusogea mbele zaidi na hatimaye kuruhusu mawasiliano ya moja kwa moja kati ya akili za Binadamu kupitia mawazo pekee jambo linaloashiria mabadiliko makubwa katika mawasiliano ya Binadamu.
Ingawa hatua hii imeibua matumaini makubwa Wataalamu wa afya na maadili wanaendelea kujadili athari na changamoto zinazoweza kujitokeza, ikiwemo masuala ya faragha ya mawazo na matumizi sahihi ya teknolojia hii katika Jamii vilevile wanatazamua mafanikio haya kuwa yanaweka msingi wa maendeleo mapya katika sayansi na tiba ya mfumo wa fahamu.
UNA MTAZAMO GANI JUU YA HILI,SHARE MAWAZO YAKO CHINI YA COMMENT SECTION,KARIBU DISCUSSION CORNER.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code