NEMC kusajili Miradi 8,058 ya mazingira
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),limesajili jumla ya miradi 8,058 ya mazingira ambapo kati ya hiyo, 5,784 ni ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na 2,274 ni ya Ukaguzi wa Mazingira.
Hayo yameelezwa leo March 24,2025 Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semester wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa Vikao 3,836 vya wataalam vilifanyika kwa ajili ya kufanya mapitio ya taarifa za TAM na Ukaguzi wa Miradi na kutoa mapendekezo ya maboresho ya masuala ya msingi ya kuzingatiwa katika taarifa hizo.
Amesema Miradi 4,570 iliidhinishwa na kupewa vyeti vya mazingira na kwamba Kati ya hivyo, 3,058 ni vya TAM, 765 ni vya Ukaguzi, huku vyeti vingine vikiwemo vya kubadili masharti 169, vyeti vilivyohamishwa umiliki 552, vyeti vya muda (PEC) 53 na cheti kilichorudishwa (certificate of surrender) ni kimoja.
"Katika kuboresha utoaji wa huduma za vibali vya TAM, Baraza lilianzisha mfumo wa kielectroniki unaotumika kusajili hadi kuidhinishwa kwa miradi ya TAM ambao umeongeza ufanisi,kabla ya mfumo Baraza lilikuwa linasajili takribani miradi 900 kwa mwaka na baada ya mfumo Baraza linasajili zaidi ya miradi 2,000 kwa mwaka, haya ni mageuzi makubwa, "ameeleza
Amefafanua kuwa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Wataalam Elekezi wa mazingira amesema katika kipindi cha mwaka 2020/21- 2024/25, Baraza limefanikiwa kusajili wataalam Elekezi wa Mazingira 1,023 na kutoa vyeti vya utendaji kwa Wataalam Elekezi 503 baada ya kukidhi vigezo kwa mujibu wa Kanuni za Usajili na utendaji wa Wataalam Elekezi wa Mazingira za mwaka 2021.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code