Nilikuwa Chanzo cha makovu ya ngozi kwa wanangu
Maelezo ya picha,Mmoja wa binti za Fatima ana mabaka kwenye midomo yake
Fatima, Mwanamke mwenye umri wa miaka 32 alitumia vipodozi vya kung'arisha ngozi kwa watoto wake wote sita, chini ya shinikizo kutoka kwa familia yake, na sasa matokeo yake anayajutia sana.
Binti mmoja hufunika uso wake kila anapotoka nje, ili kuficha kuungua kwa ngozi yake.
Mwingine aliachwa na ngozi nyeusi kuliko hapo awali, na mduara wa rangi karibu na macho yake, Fatima anasema, wakati wa tatu akiwa na makovu meupe kwenye midomo na magoti yake. Mtoto wa miaka miwili bado ana majeraha - ngozi yake imechukua muda mrefu kupona.
"Dada yangu alizaa watoto wenye ngozi nyeupe lakini watoto wangu wana ngozi nyeusi. Niligundua kuwa mama yangu anawapendelea watoto wa dada yangu kuliko wangu kwasababu ya rangi yao ya ngozi na iliniumiza sana hisia zangu," Fatima anasema.
Anasema alitumia krimu alizonunua kwenye duka la karibu, bila agizo la daktari.
Maelezo ya picha,Majeraha ya mtoto mdogo yanapona polepole sana
Mwanzoni ilionekana kufanya kazi. Bibi yao aliwakumbatia watoto wa Fatima, ambao walikuwa na umri wa kati ya miaka miwili na 16 wakati huo. Lakini baadaye wakaanza kuungua na makovu yalianza kujitokeza wazi.
Vipodozi vya Kung'arisha ngozi au kuifanya iwe nyeupe pia hujulikana kama bleaching nchini Nigeria, na hutumiwa katika sehemu mbalimbali za dunia kwasababu za urembo, ingawa tafiti zinaonyesha mara nyingi vipodozi hivyo hutengenezwa majumbani.
Wanawake wa Nigeria hutumia bidhaa za kung'arisha na kuchubua ngozi zaidi kuliko nchi nyingine barani Afrika - 77% kati yao hutumia vipodozi hivi mara kwa mara, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Nchini Kongo-Brazzaville idadi ni 66%, nchini Senegal 50% na Ghana 39%.
JE,UNAFAHAMU ATHARI ZA VITU HIVI? TUPE MTAZAMO WAKO HAPA CHINI
Credits:BBC,WHO
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code