Sababu za kuosha Miguu kila Siku,Fahamu hapa
Baadhi ya watu husugua miguu yao kila siku, huku wengine wanapendelea kumwagia maji miguu inatosha.
Lakini, je, unatunza miguu yako vya kutosha?
Unapoingia bafuni kuoga, ni kawaida kuna sehemu ambazo huziangazia zaidi na hata kuna baadhi ya viungo havipati maji ya kutosha au hupendelei kuosha.
Hata hivyo, wataalamu wanasisitiza kuwa miguu inahitaji umakini wa kutosha.
Huduma ya Afya ya Kitaifa ya Uingereza (NHS) na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) wanashauri kuosha miguu kila siku kwa sabuni na maji.
Sababu moja ya kufanya hivyo ni kuzuia harufu mbaya. Nyayo za miguu zina tezi nyingi za jasho, zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya mwili.
Ingawa jasho lenyewe halina harufu, lina mchanganyiko wa virutubishi vinavyoweza kuleta bakteria kwenye ngozi yako.
"Mguu, hasa katikati ya vidole, ni mazingira ya unyevu, joto na giza, ambayo hufanya kuwa sehemu bora kwa vijidudu kuishi," anasema Holly Wilkinson, mhadhiri wa uponyaji wa majeraha katika Chuo Kikuu cha Hull.
Zaidi ya hayo, wengi wetu huvaa viatu na soksi, hivyo hufungia unyevu ndani.
Hii ikiwa mojawapo ya sababu kwanini unapaswa kuosha miguu yako.
Kwa mujibu wa wataalamu, miguu yetu inajumuisha aina nyingi za bakteria na fangasi.
Walakini kwa sababu nyayo za miguu yako zimejaa vijidudu, hiyo haimaanishi kwamba lazima iwe na harufu au kwamba kuna chochote cha kuwa na wasiwasi.
Kama kawaida, sio idadi tu, lakini pia kuna aina ya bakteria ambayo ni muhimu.
Wakati mwingine, bakteria aina ya Staphylococcus ndiyo husababisha harufu ya miguu kwa kutengeneza kemikali zinazozalisha harufu mbaya.
Katika utafiti mmoja, watafiti waligundua kuwa kuosha miguu mara mbili kwa siku hupunguza sana idadi ya bakteria, wakati wale wanaoosha mara moja kwa siku au baada ya siku mbili, wanakutana na bakteria wengi zaidi.
Katika utafiti mmoja wa 2014, watafiti walichunguza miguu ya watu 16 na kugundua kuwa asilimia 98.6% ya bakteria waliopo kwenye nyayo walikuwa Staphylococci.
Hata hivyo, si kila bakteria kwenye miguu husababisha matatizo.Baadhi yao ni muhimu kwa afya ya ngozi yetu.
Bakteria kama Staphylococcus huunda asidi zinazohusika na harufu ya miguu.
Hata hivyo, kusafisha miguu mara kwa mara husaidia kuzuia magonjwa ya ngozi kama vile maambukizo ya fangasi, ambao husababishwa na fangasi zinazokua kwenye mazingira zenye unyevu unyevu.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code