Siku ya hali ya hewa duniani, tarehe 23 Machi
Jana tarehe 23 Machi ilikuwa siku ya hali ya hewa duniani, Tafiti mbali mbali Zinaonyesha kila mwaka kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita kumerikodiwa hali ya joto kali zaidi katika historia ya Dunia,
Pia kuna mifano ya namna mataifa mbali mbali yalivyoathirika kwa majanga kama vile moto wa msituni, mafuriko, vimbunga vikali na dhoruba zisizotarajiwa.
“Katika zama hizi za maafa yasababishwayo na tabianchi, kila mtu duniani anapaswa kulindwa na mfumo wa tahadhari ya mapema kama haki ya msingi. Pamoja, lazima tuchukue hatua sasa.”
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza “bado karibu nusu ya nchi duniani hazina mifumo ya kutabiri majanga na kuwaonya wananchi mapema. Ni jambo la aibu kwamba katika enzi hii ya kidijitali, watu bado wanapoteza maisha na riziki kwa sababu hawana mifumo madhubuti ya tahadhari ya mapema.”
Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Tahadhari za Mapema kwa Wote unalenga kuhakikisha kuwa kila mtu, kila mahali, analindwa na mfumo wa onyo ifikapo mwaka 2027. Na ili kuhakikisha hili linafikiwa Guterres amependekeza mambo kadhaa yafanyike.
Tunahitaji msaada wa kisiasa wa kiwango cha juu kwa mpango huu ndani ya nchi, msaada wa kiteknolojia, ushirikiano mkubwa kati ya serikali, wafanyabiashara, na jamii, pamoja na juhudi kubwa za kuongeza fedha.
Kuimarisha uwezo wa kukopesha wa Benki za Maendeleo ya Kimataifa ni hatua muhimu. Mkataba wa Baadaye (Pact for the Future) uliokubaliwa mwaka 2024 ulifanya maendeleo makubwa, lakini lazima utekelezwe kikamilifu. Vivyo hivyo, matokeo ya fedha ya COP29 lazima yahakikishwe.
Na mwisho ameeleza juhudi za kukabiliana na mgogoro wa tabianchi lazima ziongezwe kwa haraka. Inahitajika kupunguza kwa kina na haraka utoaji wa gesi chafuzi ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi. Mwaka huu, nchi zote zinapaswa kutimiza ahadi zao za kuwasilisha mipango mipya ya kitaifa ya kukabiliana na tabianchi, mipango ambayo inazingatia lengo la kuzuia ongezeko la joto la dunia lisizidi nyuzi joto 1.5°C.
WEWE UNAFIKIRI NINI KIFANYIKE ILI KUKABILIANA NA MABADILIKO HAYA MAKUBWA YA HALI YA HEWA?
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code