TMA yatoa tahadhari ya mvua kubwa,Siku tatu mfululizo
Mvua kubwa zinatarajia kunyesha mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuanzia siku ya Alhamisi. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewakata wananchi kuchukua tahadhari.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza angalizo la mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo katika maeneo mbalimbali nchini, kuanzia Siku ya Alhamisi, Machi 27, 2025.
Taarifa ya TMA imesema mvua hizo kubwa zinaweza kusababisha baadhi ya makazi kuzungukwa na maji. Kwa siku ya Alhamisi Machi 27, mikoa iliyotajwa kuwa na mvua ni Mara, Kagera, Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Kigoma, Tabora na Katavi.
Siku ya Ijumaa, mikoa inayotarajiwa ku[pata mvua hizo ni Mara, Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Mikoa mingine ni Singida, Dodoma, Tabora, Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa hiyo ya TMA, imesema mvua hizo kwa Jumamosi Machi 29, 2025, zinatarajiwa kunyesha Mara, Kagera, Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma na Tabora.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code