Ugonjwa wa Kutetemeka Mikono,Chanzo na Tiba
Ugonjwa wa Kutetemeka Mikono ni Ugonjwa ambao kwa jina la Kitaalam Zaidi hujulikana kama UGONJWA WA PARKINSON
UGONJWA WA PARKINSON NI NINI? DALILI ZAKE NA TIBA YAKE
Huu ni ugonjwa ambao huhusisha ubongo wa binadamu kushindwa kufanya kazi vizuri kutokana na ukosefu wa vichocheo aina ya Dopamini.
DALILI ZA UGONJWA WA PARKINSON
Je mtu mwenye Ugonjwa wa Parkinson utamjuaje?. Dalili kubwa za Ugonjwa wa Parkinson ni pamoja na;
1. Kuwa na hali ya kutetemeka Mikono
2. Kazi za ubongo kuathiriwa kama uwezo wa kutunza kumbu kumbu kupotea
3. Uwezo wa kufikiria kuathirika
4. Mgonjwa kupata shida ya kushindwa kutembea
5. Mgonjwa kujaa hofu na wasiwasi kwa muda mwingi
6. Mgonjwa kuwa na hali ya huzuni kwa kiasi kikubwa katika maisha yake
7. Mgonjwa kupata tatizo la kukosa Usingizi
8. Mgonjwa kuwa hali ya mahangaiko au kutokutulia kila mara
WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;
✓ Walio katika ukoo ambao kuna mtu mwenye shida hii,kwani huaminika kwamba vinasaba vya ugonjwa huu hurithiwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine.
✓ Wanaofanya kazi ambazo huhusisha kwa kiasi kikubwa upuliziaji wa makemikali katika mimea.
✓ Ugonjwa huu wa Parkinson hupata Wanaume zaidi ya Wanawake.
Madhara ya Ugonjwa wa Parkinson
Ugonjwa wa Parkinson ni ugonjwa wa mfumo wa neva ambao huathiri mwendo wa mwili. Madhara yake yanaweza kuathiri maisha ya mgonjwa kwa njia nyingi. Baadhi ya madhara ya kawaida ya ugonjwa wa Parkinson ni pamoja na:
- Kutetemeka (Tremor): Hii ni dalili ya kawaida ambapo mgonjwa huanza kutetemeka, hasa mikononi, hata akiwa ametulia.
- Kupungua kwa kasi ya mwendo (Bradykinesia): Harakati za mwili zinakuwa polepole zaidi, na kufanya shughuli rahisi kama kuvaa au kutembea kuwa ngumu.
- Kukakamaa kwa misuli (Muscle stiffness): Misuli huweza kukakamaa au kuwa migumu na kusababisha maumivu au kukosa unyumbulifu mwilini.
- Kutokuwa na uthabiti wa mwili (Postural instability): Mgonjwa anaweza kupoteza uwezo wa kusimama au kutembea bila kuanguka.
- Mabadiliko ya kuongea na kuandika: Kuongea inaweza kuwa polepole, kusikoeleweka vizuri, au kuwa na sauti ya chini. Kuandika kunakuwa kwa shida, na mwandiko unaweza kuwa mdogo sana.
- Tatizo la mwili kukosa balance: Wagonjwa wanapata shida katika kubalance mwili wao, na wanaweza kuanguka kirahisi.
- Madhara ya kisaikolojia: Wagonjwa wengi wa Parkinson hukumbwa na mfadhaiko, wasiwasi, na wakati mwingine matatizo ya kumbukumbu au kufikiri.
- Matatizo ya usingizi: Wagonjwa wengi hupata matatizo ya kulala, kama vile kukosa usingizi au usingizi usio na utulivu.
- Uchovu: Wagonjwa wa Parkinson wanaweza kuhisi uchovu kupita kiasi, hata bila kufanya kazi ngumu.
- Tatizo la kumeza na kutafuna: Ugonjwa huu unaweza kuathiri uwezo wa mgonjwa kutafuna au kumeza chakula, na hivyo kusababisha matatizo ya lishe.
MATIBABU ya Ugonjwa wa Parkinson
Hakuna Matibabu ya moja kwa moja ya ugonjwa wa Parkinson mpaka sasa.Ila kuna matibabu yakudhibiti Dalili za Ugonjwa huu;
Matibabu ya ugonjwa huu mara nyingi hulenga kudhibiti dalili, kwani bado hakuna tiba ya kumaliza ugonjwa wa Parkinson. Ni muhimu kwa wagonjwa kupata msaada wa kiafya kwa ushauri wa daktari.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code