Ukitumia Dawa Yoyote hakikisha una Majibu ya Maswali haya

Ukitumia Dawa Yoyote hakikisha una Majibu ya Maswali haya

#1

Ukitumia Dawa Yoyote hakikisha una Majibu ya Maswali haya.



Kabla ya kutumia dawa yoyote, ni muhimu kuhakikisha una majibu ya maswali haya:

1. Dawa hii ni ya nini? – Fahamu kwamba umepewa dawa hiyo kwa Ajili ya Nini.

2. Dawa hii haijaisha muda wake wa Matumizi(Expire date)?

3. Dawa hii inatumika vipi? – Jua njia sahihi ya kutumia dawa hyo, Mfano ni kupitia mdomoni, Ni sindano, krimu ya kupaka n.k.)

3. Kipimo gani sahihi? – Fahamu kipimo kilichopendekezwa na daktari au kilichoandikwa kwenye maelezo ya dawa, na jinsi ya kuipima.

4. Kwa muda gani nitaitumia? – Fahamu muda wa kutumia dawa hiyo hadi utakapomaliza au kupewa ushauri na daktari.

5. Je, kuna madhara au Maudhi(SIDE EFFECTS) yanayoweza kutokea? – Fahamu madhara yanayoweza kutokea baada ya kutumia dawa hiyo na namna ya kuyadhibiti mapema.

6. Je,Naweza kuitumia dawa hiyo pamoja na dawa zingine? – Fahamu kama kuna dawa au vyakula ambavyo havitakiwi kutumiwa pamoja na dawa hiyo.

7. Nifanye nini kama nitasahau kipimo? – Jua hatua sahihi za kuchukua kama utasahau kipimo cha dawa husika.

8. Nifanye nini ikiwa nitakutana na madhara makubwa? – Elewa hatua za haraka kuchukua kama utapata madhara makubwa.

9. Je, naweza kutumia dawa hii nikiwa mjamzito au ninaponyonyesha? – Fahamu usalama wa dawa hiyo kwa mama mjamzito au anayenyonyesha.

10. Ni chakula gani au vinywaji vipi ambavyo havipaswi kutumiwa pamoja na dawa hii? – Fahamu vyakula au vinywaji vinavyoweza kuathiri dawa hiyo au kuleta shida baada ya kutumia pamoja na Dawa hiyo.

Kuwa na majibu ya maswali haya kutakusaidia kutumia dawa kwa usahihi na salama.

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code