Virusi vya UKIMWI huishi kwa Muda gani Nje ya Mwili?
Hakuna jibu moja la muda gani Virusi vya Ukimwi(VVU) vinaweza kuishi nje ya mwili, kama vile kwenye damu kavu au shahawa zikiwa nje ya mwili n.k, kwani inategemea mambo kadhaa. Hata hivyo, Virusi vya Ukimwi(VVU) haviishi kwa muda mrefu nje ya mwili, na haviwezi kuongezeka yaani replication bila kuwa ndani ya binadamu(human host).
Kama nilivyosema muda wa Virusi vya Ukimwi kuishi nje ya mwili hutegemea mambo kadhaa,hivo utakutana na majibu tofauti kulingana na hali husika;
Mfano; Utakuta baadhi ya Tafiti zinasema,ndani ya muda mfupi sana, zingine ndani ya masaa kadhaa,ndani ya Siku kadhaa n.k.
Kwa mujibu wa Vituo vya kudhibiti na kuzuia Magonjwa yaani "The Centers for Disease Control and Prevention (CDC)";
Wakati hali ya joto na hali zingine zinapokuwa sawa, VVU vinaweza kuishi kwa muda wa siku 42 kwenye bomba la sindano, lakini hii kwa kawaida inahusisha uwekaji kwenye friji.
Licha ya kuishi kwa muda mrefu huu kwenye Syringe ikiwa joto lipo sawa(room temperature),Virusi hivi vya Ukimwi vinaweza kukaa kwa muda wa Siku 7 tu ndani ya Syringe endapo joto litakuwa kubwa Zaidi.
MAMBO HAYA HUATHIRI MUDA WA KUISHI KWA VIRUSI VYA UKIMWI(VVU) NJE YA MWILI;
1. Joto(Temperature): Virusi vya Ukimwi(VVU) hubaki hai na kufanya kazi wakati vikiwa kwenye baridi au joto la kawaida lakini huuawa na joto kali.
2 Mwanga wa Jua(Sunlight): Miale ya Mwangaza wa jua huweza kuharibu virusi, kwa hivyo haviwezi tena kuzaliana vikichomwa na miale hii mikali.
3. Kiwango cha Virusi kwenye fluid husika: Kwa ujumla, kadri kiwango cha virusi vya UKIMWI kilivyo juu katika fluid husika, ndivyo itakavyochukua muda mrefu kwa vyote kutofanya kazi au kuwa inactive.
4. Kiwango cha PH au Level of acidity. VVU huishi vyema zaidi kwa pH ikiwa karibu kwenye 7 na huacha kufanya kazi wakati mazingira yana asidi kubwa zaidi au kidogo.
Fahamu kwamba Virusi vya Ukimwi hupendelea mazingira ya PH ikiwa katikati ya 6.0 na 6.9. Na ndyo maana mazingira ya fluids mbali mbali za mwili kama vile Damu,Shahawa,Maziwa,au vaginal secretions, kwao ni rafiki sana.
Mazingira yakiwa yana Acid kubwa sana mfano (pH chini ya 4.0) au yana Base kubwa sana mfano (pH juu ya 9.0),Mazingira haya huwafanya Virusi kuwa inactive.
5. Unyevu unyevu kwenye Mazingira husika(Environmental humidity): Mazingira yakiwa makavu zaidi ndivo ambavyo hupunguza uwezo wa Virus kuwa active zaidi.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code