Vyakula vya kupunguza damu mwilini
Je,Vyakula vya kupunguza damu mwilini ni Vipi?
Kwa habari ya vyakula vya kupunguza damu mwilini ni ngumu kupata vyakula ambavyo huweza kupunguza damu moja kwa moja,
badala yake unaweza kuangalia vyakula ambavyo huweza kudhibiti uzalishaji wa damu au huweza kuwa na mchango kwenye mchakato wa utengenezaji wa damu kisha uvidhibiti.
Mfano; Kuepuka vyakula vyenye madini ya chuma: Madini ya chuma yanahitajika kwa ajili ya kutengeneza hemoglobini. Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye madini chuma, kama vile nyama nyekundu, spinach, na maharagwe, kunaweza kusaidia katika kudhibiti uzalishaji wa seli nyekundu za damu, na kisha kusaidia kupungua uzalishwaji wa Damu.
Kula Vyakula visivyo na wingi wa vitamini B12: Vitamini B12 inachangia katika uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye vitamini B12 nyingi kama nyama, mayai, na maziwa kunaweza kuongeza kiwango cha Damu mwilini.
Hivo basi,kupunguza kula vyakula vinavyopandisha kiwango cha damu haraka huweza kuwa njia mbadala ya kupunguza kiwango cha damu mwilini,vyakula hivo ni pamoja na;
- kupunguza ulaji wa Maharage
- Kupunguza kula nyama hasa nyama nyekundu
- Kupunguza kula mboga za majani kama vile tembele
- Kuacha kabsa kutumia juice kama vile za Beetroot,Rozella n.k
Sababu za Upungufu wa Damu mwilini:
1. Upungufu wa Virutubisho muhimu kwa ajili ya Utengenezaji wa Damu mwilini
Virutubisho hivyo ni kama vile;
- Madini Chuma(Iron): Hiki ni kiambato muhimu kinachohusika na uzalishaji wa hemoglobini, Hivo upungufu wa madini chuma huweza kusababisha Upungufu wa damu mwilini
- Upungufu wa vitamini B12: Vitamini B12 ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Upungufu wake unaweza kusababisha pia tatizo la Upungufu wa damu mwilini au anemia
- Upungufu wa folate (vitamini B9): Folate ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Upungufu wa folate pia unaweza kusababisha tatizo la Upungufu wa damu mwilini.
2. Magonjwa yanayoathiri utengenezaji wa damu: Magonjwa kama vile;
- Magonjwa ya mifupa: Magonjwa kama leukemia au myelofibrosis yanayohusisha kuathiri uzalishwaji wa seli nyekundu za damu yanaweza kupunguza uzalishaji wa damu.
3. Kupoteza damu kwa njia mbali mbali kama vile:
- Kuungua au majeraha makubwa: Majeraha makubwa au ajali ambazo husababisha kupoteza damu nyingi zinaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini.
- Kuvuja damu nyingi na kwa muda mrefu wakati wa hedhi: Wanawake wanaopata hedhi nyingi sana na kwa muda mrefu wanaweza kupoteza kiasi kikubwa cha damu kila mwezi, hali inayoweza kusababisha tatizo la Upungufu wa Damu mwilini.
- Kuwa na Vidonda vya tumbo au vidonda vya utumbo,: Vidonda vya tumbo au utumbo ambavyo vinavuja damu vinaweza kusababisha kupoteza damu kidogo kidogo lakini kwa muda mrefu, na kusababisha upungufu wa damu mwilini.
4. Magonjwa mengine ni pamoja na;
-Magonjwa ya figo: Ugonjwa wa figo unaweza kusababisha upungufu wa homoni inayoitwa erythropoietin, ambayo inahitajika kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu.
- Magonjwa ya autoimmune:
Magonjwa kama lupus au rheumatoid arthritis yanaweza kuathiri uwezo wa mwili kuzalisha seli nyekundu za damu au kushambulia seli nyekundu za damu zilizopo, na kusababisha tatizo la Upungufu wa damu mwilini.
- Ugonjwa wa bandama:
Pia Wagonjwa wengi wenye matatizo ya bandama,kama vile bandama kuvimba n.k,hupata shida ya kupungua kwa damu mwilini
- Maambukizi au magonjwa kama vile;
Ugonjwa wa homa ya Ini(hepatitis), au Ugonjwa wa malaria yanaweza kuathiri uzalishaji wa damu au kuharibu seli za damu zilizopo.
5. Matumizi ya baadhi ya dawa:
Dawa fulani, kama vile dawa za kemoterapia, antibiotics, au dawa za kulevya, zinaweza kudhoofisha uzalishaji wa seli nyekundu za damu au kuharibu seli zilizopo, na kusababisha kupungua kwa damu mwilini.
6. Hali kama Vile ya UJAUZITO
Pia Wajawazito wengi hukumbwa na hali ya Damu kupungua mwilini hasa kadri Ujauzito unavyokuwa Mkubwa.
KUMBUKA:
Kupungua kwa damu mwilini ni hali inayohitaji uchunguzi wa daktari ili kubaini chanzo na kupewa matibabu stahiki. Ikiwa unadhani unakutana na dalili za upungufu wa damu mwilini kama vile; uchovu, kizunguzungu, viganya vya mikono,Lips za mdomo,pamoja na ngozi ndani ya jicho kuwa nyeupe sana au kupumua kwa shida, ni muhimu kupata huduma za afya mara moja.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
WEWE UNA MAONI GANI JUU YA MADA HII,CHANGIA HAPA [REPLY BELOW👇]
image quote pre code