Wagonjwa wa Surua waongezeka barani Ulaya ambapo jumla ya wagonjwa 127,350 wameripotiwa kati yao watoto wakiwa zaidi ya asilimia 40%.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na lile la Afya duniani WHO pamoja na la kuhudumia watoto UNICEF yametangaza kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa surua barani ulaya ambapo jumla ya wagonjwa 127,350 wameripotiwa kati yao watoto wakiwa zaidi ya asilimia 40%.
Hadi kufikia tarehe 6 Machi mwaka huu vifo 38 vimeripotiwa.
Nchi ya Romania inaongoza kuwa na wagonjwa wengi kwa mwaka 2024 ambapo jumla ya wagonjwa 30,692 waliripotiwa ikifuatiwa na nchi ya Kazakhstan ikiwa na wagonjwa 28,147.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanahimiza utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo.
Mkurugenzi wa UNICEF katika kanda ya Ulaya na Asia ya Kati Regina De Dominicis amesema “wagonjwa wa surua barani Ulaya na Asia ya Kati wameongezeka katika miaka hii miwili – wakionesha dhahiri umbwe la kutoa chanjo….. ili kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huu hatari na unaodhoofisha, tunahitaji serikali kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuwekeza kwa watoa hudumu za afya”.
Surua ni moja ya magonjwa hatari duniani na unasababishwa na virusi vinavyoambukiza watu. Mgonjwa wa surua anaweza kupata matatizo ya kupumua, kuhara, upungufu wa maji mwilini na mgonjwa anaweza kupata matatizo ya afya ya muda mrefu kama vile upofu.
Namna bora ya kupambana na ugonjwa huu ni kupata chanjo itakayotoa ulinzi dhidi ya virusi hivyo.
#Afya News
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code